Chadema yatoa msimamo ushiriki kikao cha msajili





CHAMA kikuu cha upinzani nchini Tanzania- Chadema kimesema, hakitashiriki kikao kilichoitishgwa na ofisi ya msajili wa vyama vingi vya siasa na wadau mbalimbali wa siasa tarehe 16 na 17 Desemba 2021, jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mgeni rasmi wa kikao hicho, anatarajiwa kuwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwenyekiti wa chama tawala- Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika akizungumza na waandishi wa habari, leo Jumapili tarehe 12 Desemba 2021, makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mnyika ametoa sababu mbalimbali za kutokushiriki ni kuzuiwa kinyume cha sheria mikutano ya hadhara na kufutwa kwa kesi zote za kisiasa zinazowakabili wanachama na viongozi wa chama hicho, akiwemo Fremaan Mbowe.

Amesema, barua ya Mbowe kwenda kwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kufanyika kwa mazungumzo na Rais Samia kuijubu “mpaka sasa utekelezaji wake haujafanyika” na kwa maana hiyo “ni ngumu kwenda kwenye mazungumzo.

“Vyama vya upinzani bado havipo huru na havina haki, upande wetu Chadema tunaona rai tuliyotoa baada ya kikao cha Kamati Kuu tarehe 10 Desemba 2021 hayajafanyiwa kazi na Serikali mpaka sasa,” amesema MnyikaChadema yatoa msimamo ushiriki kikao cha msajili mwanahalisionline.com 11h CHAMA kikuu cha upinzani nchini Tanzania- Chadema kimesema, hakitashiriki kikao kilichoitishgwa na ofisi ya msajili wa vyama vingi vya siasa na wadau mbalimbali wa siasa tarehe 16 na 17 Desemba 2021, jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea). Mgeni rasmi wa kikao hicho, anatarajiwa kuwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwenyekiti wa chama tawala- Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika akizungumza na waandishi wa habari, leo Jumapili tarehe 12 Desemba 2021, makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mnyika ametoa sababu mbalimbali za kutokushiriki ni kuzuiwa kinyume cha sheria mikutano ya hadhara na kufutwa kwa kesi zote za kisiasa zinazowakabili wanachama na viongozi wa chama hicho, akiwemo Fremaan Mbowe. Amesema, barua ya Mbowe kwenda kwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kufanyika kwa mazungumzo na Rais Samia kuijubu “mpaka sasa utekelezaji wake haujafanyika” na kwa maana hiyo “ni ngumu kwenda kwenye mazungumzo. “Vyama vya upinzani bado havipo huru na havina haki, upande wetu Chadema tunaona rai tuliyotoa baada ya kikao cha Kamati Kuu tarehe 10 Desemba 2021 hayajafanyiwa kazi na Serikali mpaka sasa,” amesema Mnyika
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad