Mwanamke aliumbwa ili kuhudumiwa na sio kujihudumia. Ukiona mwanaume anahudumiwa na mwanamke fahamu kuwa huyo ni mwanamke mwenye maumbile ya kiume.
Mwanamke ni mfano wa ua zuri liliota kwenye bustani la mfalme aladini pembezoni mwa ardhi ya konya. Uwepo wa ua hilo unatunza heshima ya ardhi hiyo na himaya hiyo kwa ujumla.
Hakuna mwanaume timamu aliyewahi kubeza uwepo wa mwanamke duniani. Ndio maana hata gwiji wa wa fasihi Shabani Robert alipofiwa na mkewe aliwahi kusema:
Majonzi hayaneneki kila nikikumbukia/
Nawaza kile na hiki naona kama ruia/
Mauti siyasadiki kuwa mwisho wa dunia/
Mapenzi tuliyofunga hapana wa kufungua/
Hii ni alama kuwa mwanamke ni mtu muhimu kwenye maisha ya mwanaume.
Hadhi niliyompa mwanamke hata akiniibia kwangu naona kama nimemgawia kwa ridhaa. Wizi sio tabia ya mwanamke, ukiona mwanamke anaiba ujue msababishi ni mwanaume.
Mwanaume timamu hujinyima yeye ili mke na watoto wake wakae kwenye hali nzuri. Lakini mwanaume zuzu humfuja mke wake wa halali kwasababu ya joto la mwanamke wa nje.