Diarra awapa wakati mgumu Yanga



WAKATI mlinda mlango namba moja wa klabu ya Yanga Djigui Diarra akitimka kwa ajili ya kujiunga na kambi ya Timu ya taifa ya Mali, kujiandaa na michuano ya kombe la mataifa Afrika (AFCON), uongozi sambambamba na benchi la ufundi la klabu ya Yanga umeonekana kuangaika sokoni kutafuta mbadala wake. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mlinda mlango huyo amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 28 cha timu ya taifa ya Mali, kitakacho ingia kambini hivi karibu kwa ajili ya michuano hiyo itakayoanza kutimua vumbi tarehe 9 Januari, 2022 nchini Cameroon.

Kwenye michuano hiyo Mali imepangwa kundi F, sambamba na timu za Taifa za Gambia, Mauritania na Tunisia.

Katika siku ya jana baadhi ya viongozi wa Yanga na watu wa benchi la ufundi walionekana wakifuatilia makipa mbalimbali kwa njia ya video wakati wa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.


 
Mara baada ya kuweka kipande cha video kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Afisa habari wa klabu ya Yanga Hassan Bumbuli aliandika kuwa “Yanga inahitaji kipa ambaye ataliweka lango lao na mioyo yao salama.”

Hivi karibuni msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara alikili kuwa wapo sokoni kwa ajili ya kutafuta mlinda mlango na watakamilisha jambo hilo kabla ya kufungwa kwa dirisha hili tarehe 16 Januari 2022.

Taarifa za hivi karibuni kutoka vyanzo mbalimbali ndani ya Yanga vinaeleza kuwa benchi la ufundi la klabu hiyo limevutiwa na kiwango cha mlinda mlango wa klabu ya Mtibwa Sugar Abdultwalib Msheri ambaye anaonekana yupo kwenye kiwango bora kwa sasa.


Yanga imeamua kuingia sokoni kufuatia kubakiwa na kipa mmoja tu, Erick Johara mara baada ya kuachana na Ramadhani Kabwili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad