Katika Watu wasiojielewa, basi na @ericomondi Yupo, huyu jamaa hajielewi hata kidogo, Jamaa ni msanii wa Vichekesho ila anataka aingilie Tasnia ya Muziki, Nchini Kenya, Tena Bora angeingilia kwa Vitu vya maana na vyenye mashiko ila anaingilia kwa point za kipumbavu na za kitoto.
Anachofanya Eric Omondi kwasasa, asipozuiwa na Serikali ya Kenya Basi atasababisha Mahusiano ya Tz na Kenya Kiburudani yafe.
@ericomondi anaonesha chuki za wazi wazi kwa wasanii wa Nje Ya kenya wanaofanya Vizuri ndani ya Kenya. Eric Omondi inabidi aelewe kwamba Muziki wa Kenya hautakua baada ya kubania wasanii wa nje, ila utakua Kwa Juhudi za Wanamuziki wenyewe.
Tar 11 mwezi huu Alikiba Anashow Kenya, pia Tar 12 Harmonize Anashow Kenya, Cha kushangaza Eti Eric Omondi amekerwa na Posters za matangazo ya Shows hizo, analalamika kwamba Posters zimeonesha ubaguzi na dharau kwa wasanii wa kenya maana Picha ya Alikiba na Harmonize Zimewekwa kubwa then za wasanii wakenya ni ndogo ndogo na akaahidi kwamba Watu waliohusika kuandaa hizo events walisipobadili hizo posters basi atashawishi Raia wa Kenya wasihudhurie show hizo.
Huyu jamaa anashindwa kutambua kwamba muziki wa sasa ni biashara, Waandalizi wa Events wanaangalia faida na Sio hasara, Alikiba na Harmonize ni wakubwa kuliko Msanii yoyote pale Kenya na wanapendwa sana Pale Kenya hivyo lazima promoters watumie Sura Zao kwenye Posters.
Eric Omondi hajielewi kabisa anasahau Wema wa Watanzania, Events zake za Tanzania huwa anapokewa kama mfalme na Sijawahi kusikia Eti comedians wa Bongo Wamelaumu juu ya ujio wake.
Artist wa kenya wapambane kivyao wajitafute na wao wawe wakubwa, kipindi Wasanii wa Tz wanapambana wao walikuwa wamelala harafu sasa hivi baadhi yao wanajifanya kulialia.