Hakuna Mwanaume Mwenye Mwanamke Mmoja, Mama Usijidanganye

 


Haijalishi kuwa wewe ni dini gani, kabila gani, una kazi gani na cheo gani hapa duniani, mfumo wa uzazi wa mwanaume unafanana Na mifumo ya uzazi ya wanaume wengine wa viumbe vingine, hasa wale wenye uti wa mgongo (vertebrate) Na wanaonyonyesha (mamalia).

Viumbe walioko kwenye kundi hili wanaume wanakuwa wachache kuliko wanawake kwa sababu mbalimbali za kabla ya kuzaliwa, wakati wa kuzaliwa na baada ya kuzaliwa. Hivyo wanaume wamepewa uwezo mkubwa wa kutamani Na Kumudu kutembea Na kuzaa Na wanawake wengi kwa wakati mmoja.

Kama mfugaji anavyohitaji majogoo, mabeberu, madume wachache kwa majike wengi bandani au zizini ndivyo hivyohivyo unavyohitaji mwanaume mmoja kwa wanawake zaidi ya mmoja, na hiki kinafanyika utake usitake, ujue usijue, uambiwe au usiambiwe.

Kiuhalisia wanyama wote akiwemo binadamu wana wivu mkubwa, hawapendi kuchanganywa, lakini kama kila mume angebaki na Mke mmoja yafuatayo yangetokea kwenye jamii:

1. Wanawake wengi wasingepata mabwana, wangebaki bikra.

2. Hasira na chuki kwenye jamii ingekuwa kubwa.

3. Sonona, depression ingekuwa kubwa. Kukosa bwana kunachanganya.

4. Population, idadi ya watu ingepungua. Wanawake wengi wasingezaa kwa kukosa mbegu.

5. Idadi ya watu wanaozaliwa na hitilafu ingekuwa kubwa sana. Wanawake wangetembea na mwanaume yeyote hata mwenye hitilafu kubwa za kurithi. No choice.

6. Wanawake wangebweteka sana hadi kuwa wachafu, wavivu, na wajeuri kupindukia.

7. Wanawake wangeuana wenyewe kwa wenyewe ili wapate nafasi itakayoachwa wazi.

Asitokee mwanamke atakaejigamba kuwa yuko peke yake, hata wanaume pia kwa kiasi Fulani.

Kinachotofautiana ni idadi ya wanawake alionao mwanaume na kiwango cha kujificha, usiri mkewe au mumewe alichokuwa nacho.

Jamii ihalalishe ndoa za wake wengi ili iwe huru badala ya kuendesha mambo kwa kificho.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad