Hatima Ligi Kuu England kujulikana leo..Wachezaji Wengi Wanaugua Mafua



KLABU za Ligi Kuu England, EPL, leo Jumatatu zinakutana kujadili nini cha kufanya, kutokana na janga la virusi vya corona kuwaathiri wachezaji wengi.

Huku mechi tisa zikiahirishwa katika kipindi cha wiki moja iliyopita, ikiwa ni pamoja tano za wikendi hii zilizokuwa kwenye ratiba, klabu zinataka muda wa kujadili nini cha kufanya.

Makocha na manahodha pia watafanya mikutano yao.

Kocha wa Aston Villa, Steven Gerrard, amesema kuwa ana matumaini mkutano huo utaweka “mambo wazi” kuhusiana na “hofu kubwa zilizoko na maswali ambayo hayajajibiwa.”

Mtendaji Mkuu wa Ligi kuu England, Richard Masters ameziandikia klabu akitaka wachezaji wote wachanjwe na kusisitiza umuhimu wa kumalizika kwa msimu huu wa ligi kwa muda uliopangwa.


Naye kocha wa Brentford, Thomas Frank, alikuwa wa kwanza kutoa wito wa kusitishwa kwa mechi zote hadi Desemba 26, mwaka huu ili kuwezesha kupangwa kwa mpango mpya.

Baadhi wanahisi mapumziko yanapaswa kuwa marefu zaidi, lakini wengine kama kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp haamini hilo linapaswa kufanyika.

Taarifa ya ligi hiyo ilisema Alhamisi kwamba, inalengo la kuendelea kucheza mechi ili mradi ni salama kufanya hivyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad