Mabango ya mdhamini mwenza wa Ligi Kuu yanaondolewa Uwanja wa Mkapa ikiwa ni ishara ya kuitikia hoja ya Simba ili mchezo wa kesho uwepo.
Taarifa zinasema huenda utekelezaji wa mkataba ukasitishwa na majadiliano kuanza upya kwa kufuata taratibu.
Simba walikataa kuutambua udhamini wenza wa GSM kwenye Ligi na wakatishia kugomea mchezo wa kesho dhidi ya Yanga, lakini kupitia katika kurusa zao za mitandao ya kijamii muda mchache uliopita wamesema kila kitu kipo kwenye msitari sasa na kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi.