Hizi Hapa Tabia 3 za Mwanamke 'Ngumu Kumeza' Ambazo Hata Akiwa Mzuri Vipi Sio wa Kuoa



NI ukweli usiopingika kuwa mwanamke ndiye mhimili mkubwa katika ujenzi wa uhusiano wowote wa kimapenzi au ndoa.

Nafasi yake kubwa hujengwa na mambo mbalimbali kiasili katika maumbile kama vile uvumilivu, kuwa mkweli (kwa kiasi kikubwa) na tabia njema.

Kwa wanaotambua na kuheshimu nafasi zao kama wanawake katika ujenzi wa penzi, wataungana nami kukubali kuwa mapungufu mengi yanayojitokeza katika mahusiano na ndoa huchangiwa na mapungufu ya mwanamke.

Mshauri Boston Globe anaamini kwamba nguzo imara katika ujenzi wa uhusiano imara ni mwanamke na inapokuwa kinyume chake, ni udhaifu wa mwanamke huyo huyo ndio husababisha.


"Mwanamke ana nafasi ya kuongoza kinachotakiwa kufanyika penzini, busara katika utatuzi wa matatizo na tabia za kuvutia mwanaume na jamii kwa maana ya familia," anasema.

Aidha, pamoja na mambo mengine, tabia zifuatazo zinatajwa kama kero ambazo ni ngumu kuvumilika katika uhusiano na ikitokea kuharibia mambo yako, ujilaumu wewe mwenyewe:

1. KUONGEA SANA
Kuongea ni njia pekee ya mawasiliano na nzuri katika kuwasilisha hisia kwa mwanaume kuhusu upendo namna unavyompenda na masuala mengine ya maisha.


Lakini wapo wanawake wanaongea sana kama 'cherehani' kiasi cha kukera. Mwanaume anajuta kufahamiana na wewe kwa jinsi ulivyo mjuaji na mzungumzaji wa kila jambo bila kubagua hadhira.

Na tafiti nyingi zimeonesha kuwa mahusiano ya kimapenzi na ndoa nyingi hushindwa kufikia malengo kutokana na uwepo wa mwanamke anayesema tu kila wakati.

Hali hii huzalisha uvujaji wa siri na mipango ya ndani, lawama (zisizo na msingi), simulizi zisizo na tija za matukio ya ndugu, jamaa na majirani hadi kufikia wakati mwingine kusutwa kutokana na usambazaji wa maneno ovyo.

Hakuna mwanaume makini atakayevumilia kuwa katika uhusiano na mtu wa aina hii na unajikuta pamoja na kuwa na sifa nyingi nyinginezo, unakosa penzi endelevu na kukimbiwa kila wakati.


2. MPENZI PESA
Pamoja na umuhimu wa pesa katika kuendesha maisha yakiwemo masuala ya mapenzi, wapo wanaoamini katika ujenzi wa msingi wa uhusiano katika pesa. Hili ni tatizo.

Kipo kipande cha wimbo wa DDC Mlimani Park, dansi kisemacho 'hata njiwa ana mpenzi wake kwenye tundu ingawa njiwa hajui pesa wala shilingi'.

Ndio. Maisha ni kutafuta (pesa) lakini si kwa kuuza upendo au kutumia pesa kama fimbo ya kukuongoza kupata penzi sahihi, kwani hakuna kamwe bei ya upendo popote pale duniani.

Inashauriwa kutoegemea sana katika mahitaji ya pesa kutoka penzini, kwani msingi wa uhusiano na ndoa ni upendo wa dhati na si pesa.


Chagua kuwa 'mpenzi pesa' uone namna utakavyomaliza soli za viatu vyako kutafuta mwanaume.

Unapaswa kujiamini katika utafutaji binafsi wa maisha ili ukikutana na pesa kwa mpenzi ziwe chachu tu ya kurahisisha maendeleo utakayoyaongoza na si kutaka 'kuchuna buzi' tu kila wakati.

3. ULEVI KUPINDUKIA
Miongoni mwa burudani zinazotumiwa na wengi katika muda wa kufurahi na wapenzi ni unywaji wa pombe na wanawake wengi sana hivi sasa ni wanywaji wazuri. Haina shida!

Lakini mshauri Ann Koleen anataja ulevi kama sifa mojawapo mbaya sana kwa mwanamke, kwani ikizidi hupoteza staha, jambo ambalo ni hatari sana kwa wapendanao.

Wapo wanaotumbukia katika matukio mengi maovu bila kukusudia chanzo, kikiwa ni pombe na mara nyingi ulevi humfanya mlevi kuanika tabia zake halisi bila kificho jambo linalowafelisha wengi kufikia malengo yao kimapenzi.


Koleen anasema mwanamke anapaswa kuwa mtu makini wakati wote akifanya kila jambo kwa kiasi na ikibidi awe kiongozi wa mwanaume dhidi ya unywaji sahihi.

"Ukiwa mlevi wa kukesha kwenye baa huwezi kuwa mke mwema na hutapata mwanaume makini labda mlevi mwenzako.. ni hatari kushiriki mapenzi yenye msingi wa pombe," anasisitiza.

Pamoja na madhara mengine, mwanamke mlevi atafifisha maendeleo binafsi na ya familia kutokana na ukweli kuwa pombe, kama zilivyo starehe nyingine, zina gharama kubwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad