Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kipindi cha Shule ya Uongozi cha Mbunge Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji.
Kamati imeongeza kuwa maudhui ya kipindi ni ya upotoshaji na yanayoweza kusababisha taharuki kwa wananchi.
"Humphrey Polepole Online Television ina mapungufu ya kutokuwa na wafanyakazi wenye taaluma ya uandishi na utangazaji wa habari, jambo linalowapelekea kukiuka sheria, kanuni, misingi na maadili ya uandishi na utangazaji wa habari katika kazi zao," - Kamati ya Maudhui ya TCRA.
Maamuzi ya Kamati ya Maudhui ya TCRA imeamua kutoa onyo kali kwa kituo husika kwa aina ya maudhui ambayo imeyatoa.
Pili Kipindi cha Shule ya Uongozi kinachosimamiwa na Polepole mwenyewe kinasimamishwa kwa muda hadi pale wahusika watakaporekebisha baadhi ya maelekezo kadhaa.
Baadhi ya maelekezo hayo ni kuwa na waandishi wenye taaluma ya uandishi wa habari, kuhakikisha cvipindi vyote vinazingatia kanuni za uandishi, baada ya kukamilisha hayo kituo cha Polepole kitatakiwa kutoa taarifa TCRA.
TRCA ikijiridhisha kuwa maelekezo yote yamezingatiwa kipindi kitarejeshwa na kuwa chini ya uangalizi kwa muda wa miezi sita.
Aidha, Polepole amepewa haki ya kukata rufaa ndani ya siku 21.