Katika Hali ya kawaida zamani ilikuwa ngumu kuona picha kama hizi, wachezaji na bench la Ufundi kutoka Wapinzani wa jadi kuongea baada ya mechi
Kabla ya mechi walianza Makocha Wakuu Nabi na Pablo, wakaongea, wakabadilishana mawazo na kufurahi pamoja na hata baada ya mchezo ikawa hivyo
Hii pia ikaenda kwa Wachezaji, haswa wale waliocheza pamoja kutoka timu mbalimbali, mfano Yusuph Mhilu na Zawadi Mauya, waliongea sana pamoja
Ikaenda pia kwa wachezaji wanaotoka taifa pamoja, mfano Djigui Diarra na Saido Kanoute wote kutoka Mali wasimama uwanjani kwa muda mrefu kuongea
Kabla na baada ya mchezo, wale wachezaji kutoka Congo wote waliongea sana pamoja, walikumbatiana na kufurahi pamoja kuonesha wao hawana chuki bali ni kazi na suala la kutetea beji
Mabadiliko ya kimpira na uwekezaji yamebadili vitu vingi sana, mpaka mitazamo ya Mashabiki wa timu hizi za Kariakoo, hii ni taswira nzuri nje ya mipaka, nadhani uendelee utamaduni huu kwa mpira wetu
KARIAKOO DERBY haiwakilishi tena Waswahili wa Kariakoo bali taswira ya mpira wa Afrika Mashariki na Kati kwenye rubaa za kimataifa
Kudos 🇹🇿
@jr_farhanjr