Kifo cha mtoto aliyeuawa shuleni chazua taharuki, Wanigeria wataka haki itendeke



Zaidi ya watu 180,000 wametia saini maombi ya kudai haki baada ya kifo cha mwanafunzi wa shule ya bweni mwenye umri wa miaka 12 nchini Nigeria.

Familia ya Sylvester Oromoni inawashutumu wanafunzi wenzake watano katika Chuo cha Dowen huko Lagos kwa kumtesa kwa sababu alikataa kujiunga na kikundi cha madhehebu.

Kifo chake kimewakasirisha wengi nchini Nigeria na shule imefungwa kwa muda usiojulikana.

Katika taarifa yake, Chuo cha Dowen kilisema kijana huyo alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata wakati akicheza soka.

“Uchunguzi wa awali ulionesha kuwa hakuwa amepigana, kuonewa au aina yoyote ya shambulio dhidi ya mtoto huyo,” ilisema.

“Ninachotaka ni haki,” baba yake Sylvester, Sylvester Oromoni, aliiambia BBC News Pidgin. Akiwa anapinga maelezo ya shule kuhusu kilichotokea.

Mwanafamilia mwingine – ambaye ni binamu yake Sylvester – anaeleza tukio hilo kivingine.

Alidai kwenye Twitter kwamba wavulana watano walimkamata Sylvester, wakamfungia katika hosteli yake na kumpa kemikali ya kunywa – ambapo hakuna hata mmoja ambaye amethibitishwa na polisi, ambao wanasema bado wanachunguza.

Huku maafisa wakiendelea na uchunguzi wao, baba yake Sylvester anasema anataka Chuo cha Dowen kuwataja wanafunzi anaowashutumu kwa kumpiga mwanawe.

Baraza la kitaifa la wanafunzi linasema kuwa linaunda kamati yake ya uchunguzi.

“Marehemu alikuwa mwanafunzi kabla hajafariki na Nans [Chama cha Kitaifa cha Wanafunzi wa Nigeria] ni kwa ajili ya maslahi ya wanafunzi wote,” gazeti la Vanguard linamnukuu Kappo Olawale Samuel wa Nans akisema.

Malalamiko mengi yameenea mtandaoni, yakitaka mamlaka kuwafungulia mashtaka waliohusika na kifo cha Sylvester Oromoni na kutoa haki kwa familia yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad