Kigogo Simba Afichua SIRI "Kibu Denis Anaenda Kucheza Ulaya"

 


UWEZO mkubwa aliouonyesha straika wa Simba, Kibu Denis na kufanikiwa kufunga mabao mawili dhidi ya KMC, umemuibua Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Crescentius Magori ambaye ameweka wazi kuwa siku siyo nyingi straika huyo atauzwa Ulaya.


Kibu Ijumaa iliyopita alikuwa kwenye kiwango bora kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara pale Simba walipoibuka wa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya KMC ambapo Kibu alifanikiwa kufunga mabao mawili.


Mshambuliaji huyo alijiunga na Simba kwenye dirisha kubwa la usajili la mwezi Agosti mwaka huu akitokea ndani ya kikosi cha Mbeya City.


Akizungumza na Championi Jumatatu, Magori alisema: “Binafsi sijashangazwa sana na kile ambacho amekifanya Kibu katika mchezo wetu uliopita dhidi ya KMC, kwa kuwa ni mchezaji ambaye nimekuwa nikimfuatilia tangu akiwa Geita na Mbeya City hivyo najua ubora mkubwa alionao.


“Huu ni miongoni mwa usajili bora ambao tumeufanya msimu huu, ni kweli bado kuna vitu anapaswa kuongezewa ili awe bora zaidi kuendana na mahitaji ya timu, lakini naamini siku sio nyingi tutaanza kupokea ofa kubwa kutoka Afrika na hata Ulaya kwa ajili ya Kibu.”


JOEL THOMAS, Dar es Salaam

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad