Kigwangalla Aibuka Awapasua Vigogo Kwenye Chama



Aliyekuwa Waziri wa maliasili na utalii Dkt. Hamis Kigwangalla ameibuka na kudai kuwa kuna baadhi ya watu walikuwa wanawazushia maneno ya uongo kwenye awamu zilizopita kwenye mamlaka za juu.

Kigwangalla ambaye ni mbunge wa Nzega Vijijini amesema hayo masaa kadhaa baada ya Rais Samia kusema wazi kuwa baadhi ya viongozi wa awamu iliyopita wanalalamika kuwa awamu ya sita imeleta tena wizi na ufisadi.

"Nashukuru mama sasa ameanza kuupata ukweli wa mambo, tutafurahishwa muda si mrefu. Kuna watu walituchongea, wakatuchafua, wakatusimanga na kutusingizia mambo mengi ya uongo tu kwa kuwa walikuwa na access, sasa ya kwao yenye ‘ushahidi’ wa wazi yanajulikana! Mungu mkubwa sana" ameandika Kigwangalla kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Akiwa waziri wa maliasili na utalii Dkt. Kigwangalla aliwahi kushutumiwa kutumia kiasi cha bilioni 1 kinyume na utaratibu kitendo ambacho kinadaiwa kilichangia kutumbuliwa kwake kwenye cheo hicho.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad