Kijana Aliyeoa Bibi wa Kizungu wa Miaka 80 Kwa Magari ya Shilingi Elfu Mbili


Bernad Musyoki(35) kijana wa nchini Kenya ametaja kiasi cha mahari aliyotoa kumuoa mpenzi wake huyo wa Marekani kwa jina la Deborah ambaye ana miaka 70

Bernad katika mahojiano amesema walikutana Facebook mwaka 2017, amesema yeye ndie alianza kumtumia ombi la urafiki mwanamama huyo na baada ya wiki Bernard akarusha kete kumuomba Deborah wawe wapenzi na kufunga ndoa. Amesema Deborah hakuwa na hiyana akasema sawa na wakala viapo kadhaa huko huko inbox, Facebook


Mwaka 2018 Bernard akatakiwa aende Marekani kumuona mpenzi wake huyo lakini Bernard alinyimwa visa hivyo akawa hana jinsi wakendelea tu kuwasiliana kama kawaida

December 2020 Deborah akaamua kuja Kenya kumuona Bernard na penzi lao likazidi kupata afya na kunoga

Benard amesema watoto wa Deborah ni wakubwa kuliko yeye na mama yao huyo alipowaambia amedumbukia tena penzini na mwanaume wa Kikenya anataka kumuoa watoto wake wakawa hawana hiyana na wanawasiliana vizuri na Bernard


Kuhusu mahari, Bernard amesema wazazi wa Deborah walishafariki miaka iliyopita hivyo kwakuwa ana watoto wakubwa suala la mahari walilijadili na Deborah mwenyewe na watoto wake ambapo walikubaliana Bernad atoe mahari ya shilingi 100 za Kenya ambazo ni sawa na shilingi elfu mbili(2,000) za Tanzania, na walimwambia Bernard mahari hiyo akaitoe sadaka kanisani


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad