Kina Mbowe wagonga mwamba tena mahakamani



Mahakama Kuu divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali mapingamizi mawili yaliyotolewa na upande wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu na kupokea hati ya ukamataji mali.

Mbowe na wenzake hao, Halfan Bwire, Adamu Kasekwa na Mohamed Ling’wenya wanakabiliwa na kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Joachim Tiganga.

Uamuzi huo unahusu mapingamizi mawili ya mawakili wa utetezi katika kesi hiyo ambayo ni orodha ya vielelezo na mnyororo wa utunzaji vielelezo.

Akitoa uamuzi huo leo Ijumaa Desemba 17, 2021 Jaji Tiganga amesema mahakama inapokea kielelezo hicho na kinakuwa ni kidhibiti cha 14.

Soma maamuzi ya Jaji Tiganga

Jaji Tinganga ameingia mahakamani kwa ajili ya kutoa uamuzi wa pingamizi la mawakili wa utetezi kuhusu kupokewa kwa hati ya ukamataji mali kutoka kwa mshtakiwa wa kwanza Halfan Bwire Hassan, wakati alipopekuliwa nyumbani kwake, na kuendelea na ushahidi wa shahidi wa nane wa upande wa mashtaka.

Sasa Jaji Tiganga anaanza kusoma uamuzi akianza na hoja za pingamizi

Jaji Tiganga: Shauri hili linakuja kwa ajili ya uamuzi mdogo ambalo linahusu upokeaji wa hati ya ukamataji mali kutoka kwa mshtakiwa wa kwanza ambapo shahidi wa nane aliomba kuitoa mahakamani kuwa kielelezo cha ushahidi.

Sasa Jaji Tiganga anatoa muhtasari wa ushahidi wa shahidi wa nane jinsi walivyomkamata mshtakiwa wa kwanza Bwire na jinsi walivyokwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake mbele ya mashahidi na alivyoorodhesha mali  kwenye hati hiyo.


Sasa Jaji anaanza kuchambua hoja

Hoja ya kwanza: Hati kuongezwa ukurasa mmoja ambao hauna uhusiano na ukurasa wa kwanza kwani ukurasa huo wa pili wa hati hiyo hauna saini ya mashahidi walioshuhudia upekuzi

Hoja ya pili: kielelezo hicho kusudiwa hakina uhusiano na shauri kwa kuwa kimeandaliwa chini ya sheria isiyokuwepo na Sheria ya Makosa ya Mtandao ambayo haihusiki kwani sheria hiyo hutumika kukamata  vitu vya kielektroniki Kama kompyuta na simu lakini vitu vilivyokamatwa  ni mavazi na vitu vingine visivyo vya kielektroniki.

Jaji: Mahakama baada ya kuangalia hati hiyo imeona kama upande wa mashtaka walivyosema alichokisena wakili Mallya ni tofauti


Jaji: Fomu hii ina sheria zote mbili yàani ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na ya Makosa ya Mtandao na si kwamba Ina sheria moja kama Wakili Mallya alivyosema. Hivyo hoja ya pingamizi haina msingi.

Jaji: Kuhusu kutaja sheria ya Makosa ya Jinai kuwa ya mwaka 2002, Mahakama hii ilishaamua kuwa kutaja kimakosa jina la sheria bila kuonesha namna ambavyo upande kinzani umeathirika, hakuna madhara.


Kuongeza uzito wa msimamo huo Jaji Tiganga anarejea uamuzi wa kesi mbalimbali zilizoamuriwa na Mahakama ya Rufani kuhusiana na suala hilo kuwa kasoro hiyo kwa nyaraka kama hiyo ambayo si ya kui-move Mahakama hakuna Madhara.

Anafafanua uamuzi wa Mahakama kuwa uzito wa kutaja kwa makosa vifungu vya sheria kwa nyaraka kama hiyo kunathibitika

Jaji: Hivyo mahakama hii inatupilia mbali hoja hiyo ya pingamizi.

Jaji: Ni kweli kifungu cha 42 kilichotajwa kwenye hati hiyo cha Sheria ya Makosa ya Jinai kinahusu upekuzi wa dharura, lakini upande wa mashtaka ulieleza udharura uliokuwepo wakati wa kufanya upekuzi huo.


Jaji: Ninakubaliana kuwa huwenda kweli mazingira hayo yalikuwepo, lakini kwa namna ambavyo shahidi alieleza mahakama inaona kuwa upekuzi huo haukuwa wa dharura hivyo shahidi alilpaswa aieleze mahakama uharaka huo na alipaswa kuchukua fomu sahihi.

Jaji: Kwa kinachoonekana ni kutaja sheria isiyohusika lakini mahakama ilishaamua kuwa kutaja sheria kimakosa hakuna Madhara hivyo hoja hiyo ya pingamizi liinatupwa.

Jaji: Kuhusu kielelezo kutokuhusika kwa kuongeza ukurasa mwingine mshtakiwa.Katika mazingira hayo Mahakama inaamua kwa kuzingatia mambo yafuatayo kuwa shahidi alieleza kuwa alikwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa mshtakiwa na mbele ya mashahidi.


Jaji: Kwa hiyo kuna ushahidi kwamba upekuzi ulifanyika kwa mshtakiwa na mbele ya mashahidi. Kwa sababu hiyo Jambo hili ni la kiushahidi hivyo litaamuriwa wakati Mahakama inazingatia ushahidi wa mashahidi wengine.

Kuhusu hoja ya kutokuwepo kwa mnyororo wa utunzaji kielelezo(chain of custody


Jaji: Kwamba shahidi hajatoa maelezo ya kutosha namna gani kielelezo hicho kilimfikia tena tangu alipoachana nacho baada ya kujaza mali hizo.

Jaji: Lakini upande wa mashtaka, wakili Kidando alieleza kuwa shahidi aliweza kueleza namna alivyokipata tena na ameeleza jinsi kilivyo alivyokijaza na kwamba mpaka sasa ndivyo kilivyo na kwamba kuamua mnyororo wa utunzaji vielelezo huamuriwa mwishoni mwa shauri, hoja ambayo pia iliungwa mkono na wakili wa Serikali Abdallah Chavula

Jaji: Wakili Kibatala wa utetezi alisema kuwa ni wajibu wa shahidi kuthibitishia Mahakama kuwa kielelezo hicho hakijachezewa na akasisitiza kuwa shahidi hajaweza kufanya hivyo, huku akirejea uamuzi wa Mashauri mbalimbali ya Mahakama ya Rufani kuhusiana na hoja hiyo.


Jaji: Katika Mashauri hayo wakili Kibatala alisisitiza kuwa wakati wote ni lazima chain of Custody ielezwe

Jaji: Suala hili si jipya na mahakama hii ilishaamua kuwa chain of custody si lazima isubiri mwisho bali inaweza kutolewa hata wakati wa kupokea kielelezo Kama moja ya sehemu ya ku-establish competence ya kielelezo na shahidi mwenyewe, hivyo mahakama hii inakataa hoja za wakili wa Serikali Chavula kuwa chain of custody lazima iamuriwe mwishoni mwa shauri tu.

Jaji: Hata hivyo mahakama hii ilishaamua shahidi ili awe competent ni lazima awe ameshugulika nacho na kuna ushahidi kuwa shahidi ndiye aliyekijaza hivyo ana ufahamu nacho wa kutosha.

Jaji: Hivyo suala linalobaki ni competence ya kielelezo chenyewe


Jaji: Lakini shahidi alieleza vitu vingi namna ambavyo anakitambua kielelezo hicho ikiwemo jina na saini yake namba ya jalada, majina na saini za mashuhuda na jina na saini ya mshtakiwa pamoja na vitu vilivyomo.

Jaji: Ni kweli kuwa shahidi hakueleza kama kielelezo hicho kinaweza kuwa tempered lakini, alipooneshwa aliweza kukitambua kuwa kiko kama alivyokiandaa.

Jaji: Katika mazingira haya shahidi huyo aliweza kueleza kwa kiasi cha kutosha mnyororo wa utunzaji


Jaji: Hivyo kama kuna jambo ambalo litakuwa na mashaka basi mashaka hayo yanaweza kuletwa wakati wa cross examination (mahojiano) na mahakama itayangalia mashaka hayo.


Jaji: Kwa sababu hiyo hoja hii ya pingamizi  pia inakataliwa


Mwisho ni competence ya kielelezo

Jaji: Shahidi ameweza kutambua kielelezo hicho kwa vitu vilivyomo ikiwa  ni pamoja na jina la afisa wa Polisi.  

Jaji: Hata hivyo ni kweli kuna upungufu wa wazi lakini Wakili wa Serikali Chavula alieleza kuwa hoja hiyo inahusu substance na kwamba hakuna format inayotumika kuonesha certificate of seizure.


Jaji: Nami sikupata muda wa kutosha kufanya utafiti lakini katika upekuzi wangu nimebaini kuwa kuna format ambayo ilishapokewa mahakamani na ndio imekuwa ikitumika, kwa hiyi nakubaliana na wakili Mallya.

Jaji: Lakini pia ku na PGO inaelekeza namna ya upekuzi kuwa lazima mjumbe wa eneo husika na mashahidi waitwe ili ishuhudie kwa malengo kwa kama mtuhumiwa atafikishwa mahakamani basi waweze kuja kutoa ushahidi

Jaji: Kwa sababu hiyo Mahakama inaona kwamba fomu hiyo imetengenezwa kwa kuzingatia PGO namba 226(19) na kwa sababu hii fomu ni ya kisheria basi ilipaswa izingatia taratibu hizo za kisheria.

Jaji: Lakini kwa mujibu wa Mahakama ya Rufani, suala zima la kutoa hati hi inalenga kuonesha kuwa vitu hivyo vilivyotolewa nyumbani humo na si kwingineko.

Jaji: Hivyo Mahakama inaona kuwa saini za mashahidi ni muhimu na zinatakiwa ziwe ndani ya vifaa.

Jaji: Kwa namna ambavyo kielelezo hicho kilivyo ni wazi ina mapungufu ambayo yanampa favor mshtakiwa.

Jaji: Lakini kwa namna kielelezo hiki kilivyo kina page mbili ambazo ya kwanza imesainiwa na iko intact na ya pili haijasainiwa.

Jaji: Kwa maana hiyo mahakama hii inapokea kielelezo hicho katika page ya kwanza na ina-expunge page ya pili. Kielelezo hiki kinakuwa marked kama exhibit 14.

Wakili wa Serikali Kidando: Mheshimiwa Jaji baada ya uamuzi huo tunaomba ahirisho fupi la dakika chache ili tuweze kumuandaa shahidi.

Wakili Kibatala anapinga maombi hayo ya Serikali akidai kuwa walikuwa na muda wa kutosha tangu jana ya kumuandaa.

Wakili Kidando: Kama wenzetu wanapinga basi tunaomba shahidi huyu aende kuchukua vielelezo vingine.

Wakili Kibatala: Suala la kuleta vielelezo linaweza hata kufanywa na Askar

Sasa wakili Kidando anaendelea kumuongoza shahidi, anampa kilelezo Cha 14, (hati ya ukamataji mali kwa mshtakiwa wa kwanza, Halfan Bwire Hassan) namtaka aisome naye shahidi anaanza kuisoma.

Shahidi anataja vitu vilivyokamatwa kwa mshtakiwa kuwa ni surual za kombati, mashsti ya Jwtz, Tshir, kofia, overall jaketi yotwbya JWT nembo za majina ya Hassn B, barret, kidaftari cha ramani ya sheli za mafuta na mwisho anasoma majina na saini za mashahidi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad