Kiongozi wa upinzani nchini Benin Reckya Madougou amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani
Mahakama ya Makosa ya Uchumi na Ugaidi imempata Madougou na makosa ya kuhusika katika shughuli za kigaidi
Wakosoaji wanadai mahakama hiyo iliyoanzishwa 2016 inatumiwa na Rais Patrice Talon kunyanyasa wapinzani
Kiongozi wa upinzani nchini Benin Reckya Madougou amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani.
Kiongozi wa Upinzani Benin Ahukumiwa Miaka 20 Gerezani Kwa Ugadi
Kiongozi wa upinzani nchini Benin Reckya Madougou ambaye amehukumiwa miaka 20 gerezani kwa makosa ya ugaidi. Picha: Pan African Visions
Waziri huyo wa zamani wa haki amehukumiwa na mahakama spesheli katika jiji kuu la nchini hiyo Porto-Novo kwa makosa ya ugaidi.
Baada ya saa 20 za kusikizwa kwa kesi hiyo, mahakama ya Makosa ya Uchumi na Ugadi ilimpata Madougou mwenye umri wa miaka 47 na hatia ya kuhusika katika shughuli za kigaidi.