Na @johnharamba
Ukifika kwenye mataifa mengi yaliyoendelea, walinzi wanaohusika ndani ya viwanja mara nyingi huwa ni raia wa kawaida ambao wamepata mafunzo maalum.
Walinzi hao ambao kwa Kingereza wanaitwa ‘steward’ ni wasaidizi wa mamlaka za ulinzi, kazi yao siyo kuhukumu, ndiyo maana huwezi kukuta steward akimshambulia shabiki kwa kumpiga.
Kwetu Afrika japo siyo nchi zote kazi ya steward zinafanywa na askari na katika baadhi ya nchi hata wanajeshi wanahusika kufanya kazi hiyo.
Soka ni mchezo wa mihemko sana, ndiyo maana kuna matukio mengi ya kimihemko, kuna busara fulani huwa inatakiwa ili kudhibiti mchezo kuendelea kuwa ‘fair’.
Matumizi ya askari halisi au walinzi wa taasisi binafsi kadhaa ambao wengi wao hawana mafunzo maalum jinsi ya kudili na mashabiki au watu wa soka kwa jumla.
Ni tatizo kubwa, ndiyo maana mashabiki kupigwa na walinzi wetu katika mazingira ambayo yangeweza kuwa rafiki ni kawaida kwenye soka letu la Tanzania.
Shabiki kupata mheko na kuingia uwanjani au kumvaa mchezaji au wachezaji wakati wa kushangilia ni kawaida kutokea, popote duniani mazingira kama hayo yanatokea lakini haimaanishi kuwa ni haki ya shabiki kufanya hivyo, HAPANA KABISA.
Nini kifanyike? Shabiki iwe ni mmoja au wawili anatakiwa kuondolewa na walinzi na kurudishwa jukwaani, kama ataleta ubishi basi atatolewa nje ya uwanja au kupelekwa kwenye sehemu maalum.
Kibu Denis wa @simbasctanzania alivyofunga bao la nne dhidi ya KMC kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, jana Desemba 24, kuna shabiki alipata mihemko akaingia uwanjani kushangilia na wachezaji, lakini kipigo alichokipata kutoka kwa mlinzi hakisimuliki.
Mlinzi alimshambulia shabiki huyo kwa kupigo cha nguvu mbele ya wachezaji, huku kamera zote zikiwa LIVE.
Hakukuwa na sababu za mlinzi kumshambulia kiasi kile shabiki, kuna mamilioni ya watu wameshuhudia ‘upuuzi’ huo, inatoa picha gani kwa wadhamini, watoto…
@tanfootball na @tplboard toeni mafunzo au maelekezo kwa walinzi wanaopewa tenda za kusimamia usalama viwanjani, tofauti na hapo watu wasiokuwa na elimu ya usalama wanachafua ‘brand’ ya soka letu kiajabuajabu.