Kisa GSM Simba hatarini kupigwa faini ya milioni 1




Klabu ya Simba SC imegoma kufanya mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho wa wa Ligi Kuu Tanzania bara ambao ni mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga, sababu za kugomea mkutano huo ni uwepo wa mabango yenye nembo za GSM kwenye chumba cha mkutano.
Mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya makocha kuzungumza na wanahabari kuelekea mchezo wa Simba na Yanga utakao chezwa kesho Saa 11 jioni uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es salaam na wanapaswa kufanya hivyo ikiwa ni takwa la kanuni za Ligi Kuu Tanzania bara.

Yanga ndio walikuwa wa kwanza kufanya mkutano huo na wanahabari ambapo kocha mkuu wa klabu hiyo Nassredine Nabi ndiye aliyezungumza na baada ya kumaliza, Simba ndio walikuwa wanafata na waliitwa na kuingia ndani kwa ajili ya mkutano huo lakini walitaka bango ambalo lilikuwa na nembo mbali mbali za wadhamini wa Ligi Kuu ikiwemo ile ya GSM liondolewe.

Bango hilo halikuondolewa hivyo msafara wa Simba ambao ulikuwa unaongozwa na Ally Shantri ‘Chico’ ambaye anatoka kwenye kitengo cha Habari cha Simba akaamuru waondoke, ambapo katika msafara huo kocha Mkuu wa Simba Pablo Franco Martin alikuwepo na ndio alipaswa kuongea kueleka mchezo huo.

Kumekuwa na kutoelewana kati ya TFF na klabu ya Simba juu ya udhamini wa GSM kama wadhamini wenza wa Ligi kuu Soka Tanzania bara, ambapo klabu ya Simba imegoma kutimiza matakwa ya mkataba huo kulingana na maelekezo waliopewa na TFF mpaka wapewe ufafanuzi zaidi wa udhamini huo na wao kama klabu watanufaika vipi.


 
Kwa kushindwa kufanya mkutano huo kwa mujibu wa kanuni klabu ya Simba inaweza kupewa onyo, karipio au kupigwa faini kati ya shilingi laki 5 (500,000) hadi milioni 1 (1,000,000).

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad