KOCHA wa Simba, Pablo Franco amesema kikosi chake kina mastaa wengi wenye uwezo lakini amevutiwa zaidi na juhudi za Ibrahim Ajibu na Jonas Mkude.
Alisema baada ya kufika Simba alipata nafasi ya kufahamu kila taarifa za nyuma kwa wachezaji wake wote na aliwaambia wanatakiwa kufuta kila kitu na kuanza kazi upya chini yake.
“Ajibu aina ya maeneo kama nyuma ya mshambuliaji akitumika hapo anaweza kuwa na mchango kwenye kukaba na kupora mipira, ubora aliokuwa nao Ajibu ni mzuri pindi timu inaposhambulia anaweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga na huhusika katika mashambulizi mengi ambayo tunayafanya,”alisema Pablo.
“Muda mwingine katika mazoezi amekuwa akifunga mabao aina mbalimbali lakini anawasumbua mabeki amenivutia kama ambavyo wachezaji wengine wamefanya pia,”aliongeza
Alisema Mkude ni miongoni wa viungo bora wakabaji si Simba tu bali katika ligi nzima kutokana na uwezo wa kutimiza jukumu lake kwenye eneo hilo.
Alifafanua kuwa anaweza kukaba mashambulizi na viungo wa timu pinzani, anao uwezo wa kupiga pasi fupi na ndefu. “Jambo jema kwetu si Ajibu na Mkude bali kila mchezaji amekuwa bora na uelewa mkubwa kwa nafasi yake ila nieleze baada ya zaidi kikosi kitakuwa imara kwenye maeneo yote,” alisema. Katika hatua nyingine kocha wa zamani wa Simba, Masoud Djuma alisema katika kipindi alichofundisha soka nchini na hadi wakati huu hajawahi kutokea kiungo bora mkabaji mwenye sifa zote kama Mkude.
“Nikiwa Tanzania niliwahi kusema miongoni mwa wachezaji ambao wanauwezo wa kucheza namba sita na anakila kitu ni Mkude ambaye mpaka sasa bado hakuna zaidi yake anao uwezo wa kucheza kikosi cha kwanza na ataisaidia Simba kufanya vizuri,” alisema Djuma.
Udaku Special Blog
Nafasi za Ajira Bonyeza =HAPA=