Kumbe Nguruwe Ndiye Mnyama Safi zaidi Duniani Kuliko Wote! Jua Sababu



Je wafahamu nguruwe ndiye mnyama safi zaidi duniani? Wengi watapinga lakini ni ukweli ambao tayari umethibitishwa na wataalamu wa masuala ya wanyama.

Sifa ya kwanza inayowafanya wanayama hawa kuwa safi zaidi ni kwamba hawawezi kuchafua makazi yao kwa kinyesi.

Kumbe Nguruwe Ndiye Mnyama Safi zaidi Duniani Kuliko Wote! Jua Sababu
Nguruwe hasa wanaofugwa nyumbani hukuzwa na wakulima kwa ajili ya nyama na ngozi. Nywele zao ngumu hutumika pia kutengenezea brashi. Picha: Getty Images Source: Getty Images
Kila mara wanyama hawa hutaka eneo lao la kulala ama la kuwekewa chakula kuwa safi na huenda wasile chakula ama kukukaa kwa amani katika makazi yao ikiwa yatakuwa na uchafu huo.

Tofauti na nguruwe waliofungiwa au wanaofugwa nyumbani ambao hulazimika kunya katika makazi yao, wenzao katiki misitu au wanaoishi mbugani hawawezi kufanya hivyo. Lazima watakimbia kwenda mbali zaidi na mapango yao wanaposikia haja.


 
Tofauti pia na binadamu ni kwamba, nguruwe hawana tezi za jasho. hivyo nguruwe hujipoza kwa kutumia maji au tope wakati wa joto kali. Pia hutumia matope kama njia ya kujikinga na kuunguzwa na jua. Zaidi, matope huzuia wasiathiriwe na inzi na vijidudu.

Hali hii ya tope mwilini ndio hufanya watu wakadhani wanyama hao ni wachafu wa kutupwa.


Read also
MCA Mtarajiwa Achangiwa KSh 500 Kwenye Harambee ya Kufadhili Kampeni

Nguruwe hasa wanaofugwa nyumbani hukuzwa na wakulima kwa ajili ya nyama na ngozi. Nywele zao ngumu hutumika pia kwa kutengeneza brashi. Baadhi ya spishi za nguruwe, kama vile wale wa Asia, "pot-bellied pig", huwekwa kama wanyama wa ndani wapenzi.

Vilevile nguruwe wanatajwa kuwa wanyama werevu sana na wanaweza kupewa mafunzo na kuwa mnyama kipenzi (pet). Na wakipewa mafunzo inavyostahili, nguruwe wanaweza kufuata maagizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad