Naibu Rais William Ruto ameshikilia kwamba bado ni marafiki na Rais Uhuru Kenyatta licha ya mpasuko kati yao wakati wa muhula wa pili wa serikali ya Jubilee.
DP Ruto Akiri Kuna Uadui Kati yake na Rais Uhuru Kenyatta
DP Ruto Akiri Kuna Uadui Kati yake na Rais Uhuru Kenyatta. Picha: State House.
Ruto alikiri kwamba kuna uhasama kati yake na Rais Uhuru lakini alisisitiza kwamba hashindani naye.
"Rais Uhuru Kenyatta mbali na hii mambo yote hapa, ni rafiki yangu. Mimi na rais hatushindani; mimi nashindana na hawa wengine hapa," Ruto aliambia Inooro TV.
Ruto alisema mahasimu wake kisiasa wamajificha nyuma ya kiongozi wa kitaifa badala ya kukutana naye moja kwa moja.
"Rais Bado ni Rafiki Yangu Licha ya Yanayonipata": DP Ruto Asema Urafiki Wake na Uhuru Uko Imara
"Hawataki kushindana nami moja kwa moja. Wanasema ni wafuasi wa kupeana mikono na kujificha nyuma ya rais," aliongeza.
Uhuru awaonya Wakenya dhidi ya kumchagua Ruto
Mnamo Jumatano, Disemba 1, wakati alikuwa akipandisha mji wa Nakuru hadhi kuwa jiji, Uhuru aliwaonya Wakenya dhidi ya kumchagua naibu wake akimtaja kama mtu mwenye tamaa ya mamlaka.
Kiongozi wa taifa kwa mafumbo alimuunga mkono waziri mkuu wa zamani Raila Odinga kuwa rais huku akimshambulia Ruto.
Uhuru bila kumtaja Ruto alisema ana mbio za kumrithi akidai kuwa kampeni ni kama marathon na Wakenya watashtushwa na mbio hizo za kuingia Ikulu.
Rais alisema kampeni za ubaguzi kwa msingi wa umri ni mambo ya zamani na viongozi wanatakiwa kuchaguliwa kutokana na uwezo wao.
Hii ilikuwa ishara kwamba alikuwa akimtetea mwenzake wa handishek ambaye ana umri wa miaka 76.
Ruto akiri kuwa ananyanyaswa
Ruto awali alilalamakia kile alitaja kama unyanyasaji wa manaibu Rais wa Kenya kisiasa tangu mwaka 1963 kwa kuvuliwa mamlaka na kusalitiwa kisiasa.