Wapo wasioamini katika kipaji chake. Pia ni watu wengi waliotekwa na kipaji cha Zuchu. Licha ya kutokea familia ya wanamuziki, lakini ni wa pekee, na upekee upo kwenye ‘toni’ na akili yake.
Moja ya silaha kubwa kwa wasanii ni ‘intavyuu’. ‘Intavyuu’ inaweza kukupaisha ama kukuzika kabisa. Wengi walidharauliwa au kuheshimiwa kwa ‘intavyuu’ nzuri au mbovu na siyo kazi yake.
‘Pro. Jay’ mbali na ngoma zake, ubora wa ‘intavyuu’ zake ulimpa heshima kubwa. Hata jina la ‘Profesa’ alipewa na John Dilinga, kwa kudata na uelewa wa ‘Jay’, baada ya kupiga naye ‘intavyuu’.
Wengi hupoteza heshima kwa uchakavu wa ‘intavyuu’. Chid Benz wa sasa hivi ‘hatrendi’ kwa wimbo, bali ‘anatrendi’ kwa ‘intavyuu’. Ni msanii namba moja rafiki wa ‘maiki’ na kamera za wanahabari.
Sasa ndo Zuchu, anajua kujieleza mbele ya maiki pia ni msomi mzuri sana. Sauti tamu, shepu flan, kujieleza, Kiswahili na Kiingereza amazing. ‘Intavyuu’ ya Zuchu inavutia kuliko shepu ya Kajala.
Ukimsikiliza, utajua alihangaika ‘kujoini’ WCB, kupiga ngoma na Mondi, na hakubahatisha kuwa pale. Achana na ‘wehu’ wanaodai ‘Bwana Mkubwa’ anapumzika pale. Mbali na talanta yake, ana akili sana Zuchu.
Kipaji na ‘nyara’ ya kike sampuli hii, lazima iwe karibu. Hata mimi mngenihisi vibaya. Mfuatilie Zuchu ili ujue Mondi pia ni akili kubwa ndo maana akajua ubora wa Zuchu. Kumuelewa Zuchu usiishie kwenye sauti na midundo tu.
Kuna ‘intavyuu’ yake sikuiona kabla, lakini wiki hii nimebahatika kuitazama. Nilimpenda Zuchu kwa kipaji chake, lakini kwa ‘intavyuu’ ile sasa natamuheshimu zaidi. Toka Bububu mpaka Kwa Bibi Paje.
Aiseeeee!!! Khadija amezaa…