Huko Vaijapur taluka wilaya ya Aurangabad nchini India, hivi majuzi ndugu alimkata dada yake kichwa na pia kuukatakata mwili wake.
Kwa nini alifanya hivi, ni kwa sababu dada yake aliolewa kinyume na matakwa ya familia yake, visa hivyo sio vipya huko Maharahstra. Kiwe kisa cha Nitin Aage huko Khaeda au cha maujia ya Sonai, tunasoma au kutazama habari ya mauaji ya heshima kila wakati.
Wanaharakati wanasema idadi ya ndoa zilizo za mapenzi au ndoa kati ya makabila na matokeoa yake ya mauaji ya heshima yanaongezeka kila siku.
Lakini ni sababu zipi zinachangia kuongezeka kwa mauaji ya heshima na ni kwa njia zipi yanaweza kuzuiwa?
Wacha tuangaliwa kwanza ni kwa nini vitu hivi hufanyika.
'Mawazo ya kiume na ya kikabila'
Manisha Tokle, mfanyakazi wa kijamii huko Beed, anasema mawazo ya kiume na kikabila ndiyo sababu ya visa vya mauaji ya heshima na mawazo haya yako pande zote.
Akieleza hili anasema, ikiwa mwanamke atajiamulia, havumilii mawazo ya kiume. Iwapo mwanamke atakataa mapenzi ya mtu havumilii mawazo ya tabaka. Wasicha ni waathiriwa.
Mwanasaikolojia Hamid Dabholkar anasema kuwa wavulana na wasichana walio waathiriwa wa mauaji ya heshima ni waathiriwa wa sifa za uongo.
Watoto hawa wanauawa kwa kudai sifa za famialia zao na kadhalika. Lakini sifa hizo ni uwongo. Vitu vingi katika maisha ya kila siku huchangiwa na tabaka ambapo vijana wanauawa.
Lakini swali ni kwa njia gani visa hivi vinaweza kuzuiwa.
Wataalamu wanasema ili kuzuia mauaji ya heshima, jitihada zinastahili kufanywa katika viwango vitatu - wazazi, jamii na sheria