Laana ya Kuikejeli SIMBA Yazidi Kumtafuna Aussems..Apumulia Mashine Kenya, Namungo Wamtaka




Kocha Mkuu wa Abaluhya Football Club Leopards Sports Club ‘AFC Leopards’ ya Kenya, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ana wakati mgumu katika ligi ya Kenya.
Aussems ambaye amewahi kuhudumu katika Klabu ya Simba, kwenye msimamo wa ligi, Leopards iko nafasi ya 16 kati ya timu 18 huku ikipoteza mechi 5 kati ya mechi saba ilichochea hadi sasa, ameshinda mechi moja na kutoa sare moja.

Matokeo ya jumla hadi sasa ni kama ifuatavyo.

AFC Leopards 1-0 Tusker

KCB 0-0 AFC Leopards

AFC Leopards 0-1 Gor Mahia

Bandari 2-1 AFC Leopards

AFC Leopards 0-2 Ulinzi Stars

Sofapaka 1-0 AFC Leopards

Bidco United 1-0 AFC Leopards.

Matokeo haya unaweza kuyaweka kwenye rekodi ya WDLLLLL.

Aussems maarufu kama Uchebe alichukuliwa na klabu hiyo kwa matumaini ya kuirudisha kwenye hadhi yake ikiwa pamoja na kutwaa ubingwa wa Kigi Kuu ya Kenya ambao mara ya mwisho walishinda mwaka 1998 wakiwa chini ya kocha mtanzania, Sunday Kayuni.

Aussems aliondoka Simba SC huku akiikejeli Klabu hiyo kuwa inaongozwa na watu wasio soma, huku akiwatolewa maneno ya dharau wajumbe wa Bodi ya Klabu hiyo kubwa zaidi Ukanda wa Afrika Mashariki.

Pengine kejeli na dharau hizo kwa timu yake ya zamani Simba zimeanza kumtokea puani, kwani hivi karibuni pia alitoswa kupewa kibarua cha Ukucha Mkuu ndani ya timu hiyo baada aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes kufutwa kazi.

NAMUNGO YAMTAKA

Habari kutoka ndani ya klabu ya Namungo zinasema kuwa viongozi wameanza kufanya mazungumzo na aliyekuwa kocha wa Simba na sasa anaifundisha AFC Leopards ya Kenya, Patrick Aussems kuona namna gani watampata.

Inaelezaa kuwa Namungo tayari wamemtumia hadi mikataba yao Aussems na wamefanya mazungumzo kwa ukaribu na kocha huyo, kinachosubiriwa ni maamuzi ya pande zote mbili kulingana na hali ilivyo.

Namungo chini ya Kocha Hemed Morocco hadi sasa katika Ligi imeshinda mechi moja, sare tatu na imepoteza mechi tatu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad