MAKAMU Mwemyekiti wa Chama cha Chadema Bara, Tundu Lissu, amedai malengo ya wapigania uhuru Tanzania Bara, imesalitiwa katika kipindi cha miaka 60. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Lissu aishiye nchini Ubelgiji, ametoa madai hayo leo Alhamisi, tarehe 9 Desemba 2021 , akihutubia kwa njia ya mtandao, kongamano la miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara, lililofanyika katika makao makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mwanasiasa huyo amedai kuwa, Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, alitafsiri uhuru kuwa ni uhuru wa qananchi kuishi kwa utu na usawa, ikiwemo kutoa maoni yao, kushiriki katika vikao vya maamuzi dhidi ya maisha yao pamoja na kuwa na huru dhidi ya kukamatwa na watawala bila sababu za msingi.
“Mwalimu Nyerere alisema Watanzania hawawezi kusema kweli wako huru endapo hakuna uhuru wa kuishi kwa utu na usawa hakuna, uhuru wa kutoa maoni, kushiriki katika maamuzi yanayotuhusu na hakuna uhuru dhidi ya wanaokamatwa bila sababu na watawala. Naomba kutoa hoja kwamba, malengo haya ya uhuru yamesalitiwa,” amedai Lissu.