Magari Manne yagongana Mbozi, Lipo Basi Malori



Kutoka Mbozi Mkoani Songwe usiku wa kuamkia leo imetokea ajali iliyohusisha magari manne, malori 3 na basi la abiria kampuni ya classic lenye namba za usajili 68842 Ak 05, basi hilo linalofanya safari zake nchini Tanzania na Congo DRC limeteketea kwa moto huku Mtu mmoja akifariki na wengine 18 wakiwa majeruhi.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba amefika katika eneo hilo la tukio na kutoa taarifa kuwa basi hilo lilikuwa na abiria 13 na Wafanyakazi wa basi 6 huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa ni kutokana na ku-park barabarani kwa lori ambalo lilikuwa linabadilishwa tairi.

Mgumba amesema wamebaini kuwa kati ya majeruhi hao 8 ni raia wa Tanzania na 12 ni raia wa Congo huku akiongeza kuwa basi la classic mara nyingi hubeba mizigo mingi kuliko abiria.

#Udaku Special Blog
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad