Makamu wa rais wa zamani wa Uganda Gilbert Balibaseka Bukenya alisema ndoa hupewa kipaumbele kupita kiasi, ila hupotezea watu wengi wakati
Bukenya alimuoa mkewe Magaret Bukenya kuanzia 1974 hadi walipotalakiana majuzi
Walitengana baada ya mkewe kulalamikia uzinzi na kumburuta mahakamani akitaka talaka
Aliyekuwa makamu wa rais wa Uganda Gilbert Balibaseka Bukenya, aliyehitimisha talaka yake, alijuta kuoa na kusema kuwa ni heri angetumia ujana wake kuunda pesa.
Aliyekuwa Makamu Rais wa Uganda Ajuta Kuoa, Asema ni Heri Angetumia Ujana Wake Kuunda Pesa
Makamu wa rasi wa zamani wa Uganda Gilbert Balibaseka Bukenya alisema anajuta kuoa. Picha: Nilepsot.
Kulingana na Bukenya, ndoa hupewa kipaumbele kupindukia, ila hupotezea watu wengi wakati wao. Bukenya alimuoa mkewe Magaret Bukenya tangu 1974 hadi majuzi walipotalakiana.
Walitengana baada ya mkewe kumtuhumu Bukenya kwa uzinzi na kumshtaki mahakamani ili apewe talaka. Bukenya alisema walitengana na mkewe 2003.
Alisema hangeweza kujinyima raha za kimwili ndipo aliamua kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake hapa na pale. Mwanasiasa huyo sasa haungi mkono wazo la kuoa tena, na kusisitiza alifanya makosa kujiingiza kwenye maisha ya ndoa mbeleni.
Ruto Aashiria Kumchagua Rigathi Gachagua kuwa Mgombea Mwenza Wake 2022
“Ningalikuwa kijana, kamwe singelioa. Ningechukua muda wote maishani mwangu nikitafuta au nikiunda pesa,” Bukenya alisisitiza.
Bukenya aliyekuwa akizungumza kwenye show inayoitwa “unapologetic” aliomba msamaha kwa wale aliowaumiza moyo kufuatia matamshi aliyotoa.