Mambo Yameanza Kunoga Msimbazi Chama Kutua Simba Kabla ya X Mass, Sakho, Duncan Nyoni na Wawa Kuachwa



Kabla Ya pilau la Krismasi, Simba itakuwa imefanya uamuzi katika mambo matatu ya msingi kama kila kitu kitaenda sawa. La kwanza ni ambalo kila Mwanasimba analisubiri kwa hamu. Usajili wa Clatous Chama kurejea Simba utakuwa umekamilika na wiki hii atatua Dar es Salaam kuzitulia roho za mashabiki.

Ingawa Mwanaspoti linajua Yanga wako kwenye mazungumzo ya karibu sana na wakala wa Chama, lakini Simba iko kwenye hatua nzuri ya kumrejesha Msimbazi, staa huyo aliyekosa namba RS Berkane

Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata ni kwamba, Simba imepania kumaliza dili hilo kabla ya Jumamosi hii, lakini bado wamepanga kuachana na beki Pascal Wawa huku ubora alioonyesha kwenye dabi, ukimnusuru Onyango.

Pili, Simba itaachana na Duncan Nyoni na Pape Sakho ambao Kocha Pablo Franco amewaambia viongozi; “Wa kawaida sana hawa.”

Wachezaji hao wawili wa kigeni wameshindwa kuibeba Simba kwa ubora ambao viongozi na mashabiki walitegemea na badala yake wamekuwa wakionekana wa kawaida.

Kwenye ripoti ya Pablo aliyokabidhi wiki iliyopita amependekeza kusajiliwa nyota wapya watatu, kiungo mshambuliaji (namba nane), namba kumi ambayo nafasi hiyo imechukuliwa na Chama pamoja na straika.

Pablo amepanga kufanya mabadiliko kadhaa ya kiufundi kwenye dirisha dogo ili kurudi kwa kasi Januari ambayo amekuwa akitabiri ushindani mkali.

Simba ina uhakika kwamba Chama akitua wakiongezeka na mastaa wengine uhai utarejea kwenye timu na kutetea ubingwa wake sambamba na kufanya vizuri hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mmoja wa viongozi wa waandamizi wa Simba ameliambia Mwanaspoti kwamba wanajua kuna mawasiliano ya Chama na Yanga, lakini wao wanajua walichofanya.

“Chama anarudi kujiunga na Simba, kwani kocha kampendekeza, anamhitaji na viongozi wameona kweli umuhimu wa kiungo huyo ambaye pia yeye mwenyewe anatamani kurejea kwenye klabu yake aliyoachana nao wakati wa dirisha kubwa la usajili na katika kuelekea hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika tunamhitaji sana,” alidokeza kiongozi huyo


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad