KUFUATIA Klabu ya Simba kuugomea mkataba kati ya TFF na GSM Group wa kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara, hatimaye Msemaji wa Yanga, Haji Manara ameamua kuvunja ukimya.
Katika taarifa yao, Simba wamesema, “Hatuwezi kuanza utekelezaji wowote mpaka tupate ufafanuzi. Hadi sasa hatujapata tumelazimishwa kupokea nembo. Kuna kikao cha maandalizi kinachosimamiwa na bodi ya ligi. Nitakwenda na mawakili kupata ufafanuzi, la sivyo hatutatekeleza maagizo hayo”, Barbara Gonzalez, Mtendaji Mkuu Simba SC.
Kauli ya Manara
Unadhani Viongozi wa Makolo na Wachambuzi wao wa michongo hawakuiona hii taarifa?
Unadhani hawajui TFF (@tanfootball) wanaweza kuchukua hatua gani kwa kupuuza maelekezo yao?
Wanajua vizuri sana , ila wameamua kusudi kuset ajenda hii siku chache kabla ya mechi , ili kutuhamisha katika focus ya Jumamosi..
wao sio Mazuzu kihivyo ( Wana uzezeta wao tu), jiulize Why iwe leo,wakati mkataba umesainiwa kitambo kirefu? Mbona hawakuhoji mkataba wa NBC?
Tunajua sana jinsi walivyolobi kutaka hii mechi isogezwe mbele lakini imeshindikana, sasa leo wamekuja na barua ndefu kama mkojo wa firauni , wakiwa na ajenda ya kuharibu hii mechi isichezwe….
maudhui ya gazeti lao refu la kihayawani, Na wanachoandika machawa wao wale wale wa kila siku mitandaoni ni Zuga tu, nyuma ya pazia hawaitaki hii mechi ya tarehe 11 ( Sijui nini wamekiona)
wenye akili tushawabaini,,na tunajua wapo ktk Uchale wao wa siku zote,,ni muendelezo wa Chupli Chupli zao za kikolo ( wanacheza kuch kuch hotae)
Wananchi eeeh… let’s focus na game ya Jumamosi,,hzo porojo zao hazimzuii mwenye nyumba kulala.
Na huyo Mwenye Nyumba kasimama na Bugati ktk picha ya pili…
Ndiooooooo anaitwa GHALIB SAID MOHAMMED muite GSM 👌🦾
Porojo tupa kule, Njooni Jumamosi tumalizane,,,Barua za michongo haziwasaidii kwa sasa… Mpo Makolo??