Dar es Salaam. Marais wa nchi nne pamoja na marais wastaafu watatu wamehudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru zinazoendelea sasa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Desemba 9,2021.
Marais hao ni wa Kenya, Rwanda, Msumbiji pamoja na visiwa vya Comoro na wengine ambao hawakuweza kufika wametuma wawakilishi.
Kati yao, alianza kuwasili rais mstaafu wa Malawi Joyce Banda ndiye na kufuatiwa na rais mstaafu wa Msumbiji aliyeambatana na Waziri wake wa Afya.
Baadaye aliwasili rais mstaafu wa Botswana aliyeambatana na waziri wa mambo ya nje na baadaye aliwasili waziri mkuu wa nchini DRC Congo.
Aliyefuata alikuwa rais wa visiwa vya Comoro, Azali Assouman, rais wa Msumbiji, Philipe Nyusi, rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na wa mwisho alikuwa rais wa Rwanda Paul Kagame.
Viongozi wengine waliowasili ni rais wa mahakama ya Afrika, mabalozi wa nchi mbalimbali na wakurugenzi wa wizara.