Masalio ya kale ya farao wa Misri yamefanyiwa utafiti kwa mara ya kwanza katika milenia baada ya "kufunuliwa" kidijitali.
Masalio hayo ya Amenhotep I, ambaye alitawala kutoka 1525 hadi 1504 KK, yalipatikana kwenye tovuti huko Deir el-Bahari miaka 140 iliyopita.
Lakini wanaakiolojia waliacha kumfungua kifunika uso chake au bandeji usoni kwa ajili ya kumuhifadhi.
Uchunguzi wa kutumia kompyuta (CT scan) sasa umefichua habari isiyojulikana hapo awali kuhusu Farao na mazishi yake.
Dk Sahar Saleem, profesa wa radiolojia katika Chuo Kikuu cha Cairo na mwandishi mkuu wa utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Frontiers in Medicine, alisema walimuonesha Amenhotep akiwa na umri wa miaka 35, wakati alipofariki.
"Alikuwa na urefu wa takriban 169cm (5ft 6in), alitahiriwa, na alikuwa na meno mazuri.
Ndani ya sanda yake, alivalia shanga 30 na mshipi wa kipekee wa dhahabu wenye shanga za dhahabu," aliiambia PA Media.
"Amenhotep anaonekana kufanana na baba yake kimwili: alikuwa na kidevu chembamba, pua ndogo nyembamba, nywele zilizopinda, na meno ya juu yaliyotoka kidogo."
Hata hivyo, Dk Saleem alisema hawakuona majeraha au ulemavu wowote kutokana na ugonjwa ambao ungewawezesha kutoa sababu ya kifo chake.
Watafiti hao waliweza kupata ufahamu juu ya kuangamizwa na kuzikwa kwa Amenhotep, ambaye alikuwa mfalme wa pili wa Enzi ya 18, ikiwa ni pamoja na kwamba alikuwa farao wa kwanza kukunja mikono yake kifuani mwake na kwamba, katika hali isiyo ya kawaida, ubongo wake haukuondolewa.
Pia walihitimisha kwamba masalio hayo ya kale "yalirekebishwa kwa upendo" na makasisi wa karne ya 21 ya Dynasty, ikiwa alitawala karibu karne nne baada ya kifo hiki.
Uchunguzi huo wa komputa ulionesha kuwa binadamu huyo wa kale aliuguza majeraha kadhaa kabla ya kifo ambayo yanawezekana yalisababishwa na majambazi.
Pia walionesha kwamba makasisi waliweka vizuri kichwa na shingo iliyojitenga kwenye mwili kwa kamba, walifumuweka sawa kasoro kwenye upande wa tumbo walifunga kwa mkanda na kuweka shanga mbili chini, na kuzungusha mkono wa kushoto uliojitenga kwa mwili.
Dk Saleem alisema vito na shanga zilizoonekana kwenye skani zilikanusha nadharia kwamba mapadri waliviondoa ili vitumiwe na mafarao wa baadaye.
Masalio ya kale ya Amenhotep I yalizikwa upya na makasisi katika Hifadhi ya Kifalme ya Deir el-Bahari, makaburi yaliyo karibu na mahekalu ya Luxor, ili kuyaweka salama.