Mchawi wa Bongo FLAVOR ni Msanii , Shabiki au Media ?

 


Ngoja niwasaidie kuelewa MUZIKI na Aina yake naongea Kama mwandishi wa MUZIKI .. changamoto ata sisi waandishi tunapitia ..mtu anakupa beat ya amapiano au ya bolingo af anakwambia niandikie isound Kama ya mtu fulani ..kwavile analipia mwandishi atajitaidi kuweka signal flan za asili za Aina iyo ya muziki ili tu iendane na nyimbo ambazo zipo kweny trend ..


Wasiojua bongo flavor .. beat lake hasa linalo tambulisha bongo flavor japo Kuna beats tofauti toafuti ila ukisema niandike muziki ambao ni 100% bongo flavor nitatafuta beat ya Mac muga ya alikiba ..then nitachukua beat ya marioo inatosha chukua beat la samir nitapoa chukua beat ya diamond mbagala izi beats uki play azi sound ki Zanzibar au kibara au taifa lolote lile ni pure bongo flavor .


Ili nchi iwe na identity ya MUZIKI lazima iwe na muziki wa taratibu nawa haraka haraka Kama ilivyo SEBENE na RUMBA Kama ilivyo AFROBEAT na high Life nikimahanisha play wimbo wa wizkid then play nawa Mr flavor au tecno najua ushaelea ukienda SA kulikuwa na kwaito ambayo saiz imezalisha amapiano pia wananyimbo zao za taratibu ambazo pia zinaasili ya SA tafuta wimbo wa mafikizolo wimbo unaitwa nemlanje ..utaelewa


Kama ilivyo hip hop na danceall

R&B na pop

Hip hop imezalisha trap

Pop imezalisha electric music


Bongo flavor hatukua namziki asilia wa haraka haraka tulipotaka kufanya mziki wa haraka tulikua tunahngukua kwenye bolingo au kwaito .. sikiliza ngoma za mr nice , h baba bushoke zilikua na mahadhi yakikongo wasanii walikuw wakikata mauno .. sikiliza ngoma za nyuma kidogo sumali hakunaga .. diamond nataka kulewa tuliangukia kwenye kwaito..


Kwasasa tumeshapata muziki wa haraka haraka ambao ni SINGELI Aina haja ya msanii wakibongo kutoa album nzima ya amapiano .. Kama ilivyokua mtu akipiga sebene lazima anyanyuke acheze ata SINGELI inaiyo nguvu yakumtoa mtu kwenye kiti ..


Kama zilivo high Life , pop , electric music , danceall , Latina music, amapiano, sebene etc..


Japo sipingi sounds zingine kutumika ila lazima bongo flavor na SINGELI tuzipe kipao mbele pia.. niaibu msanii wakibongo ku perform amapiano, sebene , afrobeat etc.. kwenye majukwaa yakimataifa bila kuperform wimbo wowote wa bongo flavor au SINGELI ..


Nini mtazamo wako juu ya ili ?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad