Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imesema Mvua kubwa inatarajiwa kuikumba Mikoa sita katika kipindi cha siku tatu kuanzia leo, Jumamosi mpaka Jumatatu ambayo inaweza ikaleta madhara kwa Wananchi wa maeneo hayo
Mikoa iliyotajwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata mvua hizo ni Dar es Salaam, Tanga, Pwani (kikiwamo kisiwa cha Mafia), #Zanzibar, Morogoro na Lindi
TMA imewataka wananchi na sekta husika kuchukua tahadhari na kuzingatia utabiri walioutoa.
#Udaku Special Blog