Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana na klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC Bernard Morrison ameanza kujihami na changamoto za kubambikiwa kesi ya kukutwa na Maambukizi ya Virusi vya Corona.
Morriosn ameonyesha hali hiyo kwa kuweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagarm inayomuonesha akiwa Uwanja wa Ndege, amevaa Barakoa hadi machoni.
Kiungo huyo ambaye aling’aa kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows ya Zambia, anahofiwa huenda akababikiwa kesi ya kukutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona atakapofika mjini Lusaka.
Morisson ameandika: Najaribu kujikinga kabla hawajasema nina maambukizi ya vya Virusi vya Corona nikifika Zambia
Morrison alifunga mabao mawili kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza dhidi ya Red Arrows, Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam huku bao lingine likifungwana Mshambuliaji Meddie Kagere.
Simba SC inatarajia kuondoka leo Ijumaa (Desemba 03) kuelekea Lusaka-Zambia, tayari kwa mchezo wa Mkondo wa Pili wa Kombe la Shirikisho Afrika, utakaochezwa Jumapili (Desemba 05).
Katika mchezo huo kikosi cha Simba SC kitalazimika kusaka ushindi ama matokeo ya sare ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya Makundi, huku wenyeji wao Red Arrows wakihitaji ushindi wa mabao 4-0 na kuendelea.