Mrembo mwenye figure matata kutoka Bongo land/ tanzania @poshyqueeen amepokea mapokezi ya namna yake kutoka kwa members wa KondeGang wakiwa nchini Kenya katika shughuli zao za kimuziki.
Mapokezi hayo yalianza kutoka kwa official Dj wa mwanamuziki Harmonize @djsevenworldwide kwa kuvalia t-shirt yenye picha ya mrembo huyo, kabla ya kuhamia katika mtandao wa Instagram, ambapo pia Boss wa lebo hiyo @harmonize_tz aliweza kumkaribisha rasmi mrembo huyo katika familia yao.
Bado haijajulikana ama kuwekwa wazi kama kuna uhusiano wowote kati ya mrembo huyo na official Dj wa harmonize #DjSeven