Mrithi wa KIPA Diarra Anayeondoka 'aivuruga' Yanga



WAKATI Yanga ikipangwa kuanza kampeni ya kuwania ubingwa wa Kombe la Mapinduzi Zanzibar kwa kuvaana na Taifa Jang'ombe Januari 5, mwakani, uongozi wa timu hiyo uko katika mipango ya kunasa saini ya golikipa mzawa ili kurithi mikoba ya Djigui Diarra atakayekwenda kushiriki fainali za Kombe la ...

Mataifa ya Afrika (AFCON 2022), nchini Cameroon akiwa na kikosi cha Mali.

Mohammed Makaka wa Ruvu Shooting, Abdultwalib Mshery (Mtibwa Sugar) na Haroun Mandanda wa Mbeya City wanatajwa kutua katika klabu hiyo ambayo tayari imeshatangaza kuachana na Ramadhani Kabwili.

Taarifa kutoka katika klabu hiyo zinasema Yanga inahitaji kuimarisha eneo hilo kwa sababu baada ya Diarra kuelekea AFCON, timu itabakia na kipa mmoja tu, ambaye ni Erick Johora.

"Diarra hana wa kumpa ushindani, tumeingia sokoni kusaka mtu ambaye atakuwa bora langoni hata asipokuwapo, akiwa katika majukumu ya kuiwakilisha nchi yake, hatutakuwa na presha kuhusu mbadala wake," kilisema chanzo chetu.


Chanzo hicho kilisema nafasi ambayo 'inawaumiza kichwa' na wanahitaji kuiimarisha zaidi katika kipindi cha dirisha dogo la usajili ni ya golikipa.

“Suala la usajili limeshafika kwa uongozi na nina imani kila kitu kitaenda vizuri, kazi yangu kubwa kwa sasa ni kuhakikisha tunaendelea kuimarika na kutafuta pointi muhimu katika michezo hiyo iliyopo mbele yetu,” Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga alisema.

Aliyekuwa kiungo wa Azam FC, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ na winga wa Biashara United, Dennis Nkane wameshakamilika usajili wa kujiunga na Yanga.


Wakati huo huo, katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi, Yanga imepangwa katika Kundi B ikiwa na Taifa Jang'ombe na KMKM huku Simba ikiwa Kundi C pamoja na Selem View na Mlandege wakati Kundi A linaundwa na Azam FC, Namungo, Yosso Boys na Meli 4 City.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad