🔉Baada ya uwekezaji kufanyika kwenye Ligi Kuu soka Tanzania Bara ambapo NBC ndio main sponsors na baadae GSM kuweka pesa pia kama Co Sponsors
🔉Klabu ya Simba ilipokea nembo kutoka Mamlaka za soka nchini kwamba kuelekea Derby wanapaswa kuvaa nembo nyingine ya Mdhamini mwenza kwenye Ligi
🔉Simba waliandika barua Desemba 2, kueleka kwa Mamlaka husika kuhitaji ufafanuzi kuwa inawezekana vipi kisheria wakatekeleza hivyo na hawakupokea majibu zaidi ya kuambiwa wavae
🔉Msimamo wa Simba mpaka sasa ni kuwa hawatotumia nembo hizo mpaka pale wakipata ufafanuzi wa kisheria na unaoleweka nje na hapo haiwezekani
🔉Siku mbili kabla ya derby ya Kariakoo kutakuwa na kikao kati ya Simba, Yanga na TPLB kuelekea mchezo huo ila CEO wa Simba atafika na jopo la Wanasheria kuulizia Uhalali wa kutumia nembo nyingine tena kwenye jezi zao nje na ile ya NBC
🔉CEO Barbra anafahamu vyema kuwa kupinga kuweka hiyo nembo nyingine ni faini ya million 3 kwa mechi moja mpaka tatu na kisha adhabu kubwa ni kushushwa daraja
❗Msimamo wa Simba ni kupata ufafanuzi wa kisheria na waambiwe wanatekeleza hivyo kwa kifungu kipi?? That's it for now
[Ufafanuzi wa Voicenote inayotembea kwenye WhatsApp ambayo wengi hawajaielewa taarifa kamili]
TUKUMBUKE| Takwa la GSM ilikuwa ni kukaa upande wa kushoto wa jezi za timu zote, ndivyo GSM walivyotaka na mkataba ulisainiwa kwa masherti hayo