Muda si Mrefu Baba LEVO Atafukuzwa WCB, Dharau Kwa Bosi Wake Zimedhidi



Mpaka sasa @officialbabalevo ameonesha dharau kubwa sana kwa Diamond na WCB kwa Ujumla.

Rejea haya;
Amewahi kujibizana vibaya na kumtukana Mheshimiwa Babutale mbele ya Umma bila kutambua kwamba, tale anauwezo wa kumshawishi Diamond, amuondoe chawa huyo pale WCB na Wasafi Fm.

@officialbabalevo amewahi kumuombea Diamond afe ili auze cheni aliyopewa kama zawadi, cheni hiyo alipewa na Diamond. Tujikumbushe....Diamond amewahi kumzawadia gari Babalevo, lakini halikudumu sana, Babalevo akaliuza, Inawezekana baada ya Diamond kusikia hili suala kuwa gari limeuzwa nahisi alikasirika na kumuonya babalevo. Ndio maana sasa hata kipindi Babalevo anapewa cheni akaongea yale maneno kuwa anamuombea Diamond afe ili auze cheni aliyozawadiwa.

@officialbabalevo ameonesha dharau kubwa kwa kampuni ya @wasafibetofficial , anadai kuwa kampuni hiyo ni ndogo ndogo huwezi linganisha na kampuni ambayo yeye anafanya kazi.

Sasa yote haya yanaendelea lakini bado wanamvumilia huyu jamaa, labda kama wanamtuma ili achafue hali ya hewa ili waendelee kutrend, lakini kama hatumwi, aisee life span yake pale Usafini ni fupi sana, Dharau Zimezidi...........Uchawa na uropokaji wake wa Bila kufikiria Utamponza.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad