Kila siku saa tatu asubuhi, Ilona Taimela aliwasalimia wanafunzi wake na kuwaelezea masomo yao ya siku
atiba yake ya siku ilidumu kwa takriban mwaka mmoja kuanzia Mei 2020 na alishirikiana na waalimu wengine wengi aliokuwa akifundisha nao bila kuwepo.
Mbali na wanafunzi wa Bi Taimela wanafunzi walikuwa wakifundishwa katika jela za kambi kaskazini-mashariki mwa Syria- mbali na dawati lake nchini Finland.
Kupitia ujumbe alioutuma kupitia WhatsApp, aliwafundisha masomo Hisabati, Jiografia katika lugha ya Kiingereza na kifinland.
Wanafunzi wake walikuwa ni Wafinland 23 wanaoishi katika kambi ya al-Hol , yenye mahema makubwa iliyowekwa kwa ajili ya watu wenye uhusiano na kundi la Isramic State.
Takriban watu 60,000 wanaishi ndani ya kambi hiyo, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto kutoka nchi makumi kadhaa, wakiwemo wanaotoka Ulaya.
Baadhi ya watoto hao walikuwa ni wanafunzi wa Bi Taimela.
" Japokuwasikuwafahamu watoto hao, walikuwa na haki ya ya kupata elimu," aliiambia BBC.