Mwanamke Afikishwa Mahakamani kwa Kukosa Kurejesha Pesa Alizotumiwa Kimakosa




Nancy Chonge Chepkwemoi alishtakiwa kwa kuiba pesa hizo kutoka kwa Vincent Maina Wambutu mnamo Novemba 27 kinyume na kifungu cha 268 (1) cha kanuni ya adhabu.

Wambutu alikuwa akituma pesa kutoka kwa akaunti yake ya benki hadi Mpesa lakini akaingiza nambari isiyo sahihi na kutuma pesa hizo kwa Chepkwemoi kimakosa.

Hakujua hadi siku iliyofuata alipowasiliana na Chepkwemoi na kupata simu yake ikiwa imezimwa. Akamtumia ujumbe mfupi.


 
Wambutu kisha aliripoti kisa hicho kwa benki akiomba kurejeshewa pesa hizo lakini baadaye akaambiwa itakuwa vigumu kwani tayari hela hizo zilikuwa zimetolewa.


Chepkwemoi aliwasha simu yake baada ya siku tatu lakini hakuwasiliana na Wambutu wala kumrejeshea pesa.


Wambutu aliripoti kisa hicho katika kituo cha polisi cha Parklands na Chepwkemoi alifuatiliwa na kukamatwa.

Alikanusha mashtaka mbele ya hakimu mkazi mkuu Renee Kitangwa wa mahakama ya Kibera.

Aliachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu KSh 50,000. Kesi hiyo itatajwa Desemba 21.

Mwezi Agosti TUKO.co.ke mwanamke mfanyabiashara kutoka jijini Nairobi alijikuta matatani baada ya kukamatwa akitoa pesa alizotumiwa kwa akaunti yake ya M-Pesa kimakosa.


 
Elizabeth Karimi Muthoni alikabiliwa na shtaka la kuficha pesa alizotumiwa kimakosa kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya Uhalifu wa Mtandaoni ya 2018.

Jumla ya Ksh 271, 200 zilitumwa kwa akaunti yake ya M-Pesa na Bakar Hussein Mohamed kutoa huko Kitengela, Kaunti ya Kajiado, mnamo Julai 14.

Alipowasili mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Kibera Philip Mutua, mshtakiwa alikiri kutekeleza kosa hilo.

Akaunti ya wakala inamilikiwa na Muthoni, ambaye biashara yake iko Kitengela.


Benki ya eneo hilo ilikuwa imekubali kumrejeshea Mohammed pesa hizo kwa akaunti yake lakini tayari mtuhumiwa alikuwa amezitoa pesa hizo tayari.

Aliiambia korti kwamba alitoa kiasi fulani cha pesa hizo ila alikuwa kwenye mazungumzo na Mohammed ya jinsi atakavyomrejeshea pesa hizo.

Korti ilimtoza faini ya KSh 200,000 baada ya kukiri mashtaka au endapo akashindwa kulipa pesa hizo basi atalazimika kutumikia jela miaka miwili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad