Katibu wa siasa na uenezi (CCM) mkoa wa Njombe Ndug. Erasto Ngole amezungumza na vyombo vya habari na kueleza masikitiko ya Chama hicho mkoa wa Njombe kutokana na matamshi ya Spika wa bunge Job Ndugai mitandaoni yanayoonekana kumdhoofisha Rais Samia.
Ngole amesema Chama hicho kinatambua uwepo wa kundi la watu linaloonekana kukinzana na kazi anazofanya Rais Samia na kuwataka kuacha mara moja kwa kuwa hawapo tayari kuendelea kuona Rais Samia ambaye ni mwenyekiti wa Chama chao akiendelea kudhoofishwa na wachache.
“Tunajua kuna kikundi ambacho kipo na Mh,Ndugai hakijaridhika Mh.Samia kuwa Rais.Samia amepewa Urais na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nab ado sisi tuna sema hatuna Rais mwingine 2025 zaidi ya Samia”Amesema Erasto Ngole
Aidha amesema Rasi samia ana hofu kubwa ya Mungu ndio maana amekuwa muwazi katika shughuli anazotekeleza kwa kutumia mikopo.
“Mama Samia ana hofu ya Mungu ndio maana kila mkopo unaokuja anauweka wazi,ni serikali ngapi huko nyuma zimekopa na watanzania tulikuwa hatujui,leo mama anachofanya anaweka wazi halafu Ndugai analeta kelele”Alisema Erasto
Vile vile ameseama kuendelea kudharau na kupiga kelele juu ya ufanyaji kazi wa Rais Samia ni kuzidi kumdhoofisha na kuomba kumuacha afanya kazi kwa kuwa wapo viongozi wengine akiwemo Spika Ndugai waliokuwepo katika awmu zilizopita na walifanya mambo mengi bila kusumbuliwa
“Bunge lililopita Ndugai alikuwa Spika wa Bunge,serikali imekopa vingapi huko nje na viko kimya hakuna anayejua,je aliinuka na kusema chochote,kwanini iwe leo ni lazima tumuunge mkono Rais Samia”amesema Ngole
Hata hivyo amesema anashangazwa na kitendo kilichofanywa inagali yapo mambo mengi yanayofanywa kinyume na Spika huyo
“Ndugai watanzania tumekuheshimu,tumekupa bunge linda heshima uliyopewa pamoja na hayo unaendesha bunge kibabe unavyotaka wewe ufuate kanuni,lakini humo bungeni una wabunge wasio na vyama umewatoa wapi? Katiba ya nchi inasemaje.Muache mama atafute pesa” amebainisha Ngole
Ngole amempongeza Rais Samia kwa kuendelea kuisimamia serikali na kufikisha fedha nyingi za miradi mkoani Njombe ikiwemo miradi ya madarasa ambayo imekamilika kwa 100% kwa sasa na kukabidhiwa kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya.
Desemba 28 katika mkutano mkuu wa pili wa wanakikundi cha Mikalile Ya Wanyusi uliofanyika jijini Dodoma, Ndugai alitetea uamuzi wa Bunge kuanzisha tozo za miamala ya simu, kuliko kuendelea kukopa.
“Juzi mama ameenda kukopa 1.3 trilioni. hivi ipi bora. Sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru kuzidi kukopa na madeni au tubanane banane hapa hapa, tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa makubwa haya yasiyoeleweka. Ni lini sisi tutafanya wenyewe ‘and how’ (na kwa vipi),” alisema Spika Ndugai.
“Tutembeze bakuli ndio heshima, tukishakopa tunapiga makofi, sisi wa kukopa kila siku,’ amesema Ndugai huku akitetea tozo kwamba; “Tukasema pitisha tozo anayetaka asiye taka pitisha tozo, lazima tuanze kujenga wenyewe, nani atatufanyia, yuko wapi huyo mjomba, tukapitisha.
“Sasa 2025 mtaamua mkitoa waliopo nayo sawa waje watakaokuwa kazi yao kwenda kukopa, endapo hiyo namna ya ku-run nchi (kuongoza nchi) hivi sasa deni letu ‘seventy trilioni’ (Sh70 trilioni). hivi nyinyi si wasomi ‘is that healthy’ (hiyo ni afya). Kuna siku nchi itapigwa mnada hii,” alihoji Ndugai kwenye mkutano huo wa kimila wa kabila la Wagogo.
Hata hivyo, kwa upande mwingine, Rais Samia akizungumza Desemba 28 katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa SGR uliofanyika Ikulu ya Dar es Salaam, amesema Serikali itaendelea kukopa ili kukamilisha ujenzi wa reli hiyo.