Niko tayari Kusamehe - Rais Samia



Niko tayari Kusamehe - Rais Samia
RAIS Samia Suluhu Hassan amesema yuko tayari kusamehe ili kuzika tofauti za kisiasa na kufungua ukurasa mpya wa kuendesha taifa hata hivyo ametaka viongozi wa vyama vya siasa kuzingatia sheria za nchi.

Kama mlezi, kama mkuu wa nchi. Nina jukumu na wajibu wa ulezi. Nakama mlezi natakiwa kuwa mvumilivu msikivu na mwenye kusamehe na niko tayari kufanya yote haya. Nita sikiliza nitavumilia mnayo niambia, mnayo nikosoa na niko tayari kusamehe ili tuende vyema. Lakini mambo haya ni pande mbili. Mimi nimesimama, ninasema mbele yenu wengine wako kwenye vyombo vya habari wananiona na ulimwengu unanitizama niko tayari kuvumilia kustahamili na kusamehe. 

Demokrasia ni kuheshimu Sheria. Unapo heshimu sheria ndipo demokrasia inapokuwa, lakini ndipo inapoleta heshima. Heshima ya mtu inakuja kwa kuheshimu Sheria za nchi. Unapovunja sheria za nchi, heshima yako haita heshimiwa. Serikali haitakuheshimu. 

Lazima pia utambue unapotumia Uhuru wako mwisho wa Uhuru wako inaanza heshima ya mtu mwingine


 
Isingekuwa uvunjifu wa Sheria leo isingemlazimu (Zitto Kabwe) kuomba hapa yule mwenzetu (Freeman Mbowe) muachie. Lakini unapovunja sheria unajivunjia heshima, na serikali inashindwa kukuheshimu. Naomba tufanye kazi kwa kuheshimu sheria.

Waswahili wanasema, ‘Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba’ ingawa kusameheana nako kupo.

Ili kuifanya demokrasia inawili lazima tuende na matakwa ya sheria. Kama sheria tunazikubali inapitishwa na bunge wananchi wanazikubali lazima tufuate sheria. Hivyo niviase vyama vya siasa na vya kiraia kuheshimu sheria ili uhuru na amani kwenye nchi yetu iweze kutamalaki.


Nina sisitiza tujadili kwa kuongozwa na kuzingatia historia mira, tamaduni, slika na desturi zetu na mkutadha wa hali ya kiuchumi ya nchi yetu. Kuna mazoea ya kuangalia hali ya demokrasia ya vyama vingi kwa kulinganisha na nchi ambazo tunatofautiana kihistoria kiutamaduni, maendeleo ya nchi na hata mktadha wa kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi. 

Jambo hili sio sahihi. Demokrasia ya wenzetu hata kule mfumo huu uliko asisiwa na wenyewe wanayao na demokrasia yao haiwezi kuwa sawa na yetu na ya kwetu haiwezi kuwa sawa na yao. Ni kwasababu demokrasia haina fomula. Kwamba ukichukua moja kwa moja ni mbili na haibadiliki.

Demokrasia inaenda na historia ya nchi uwezo wa kiuchumi, mira na desturi za nchi, mwenendo wa uchumi. Huwezi kuchukua demokrasia ya taifa lenye miaka 200+ ukalinganisha na demokrasia ya taifa la miaka 60. Sisi bado tunaitwa wachanga wa demokrasia.

Kwahiyo tunakwenda kwa uchanga wetu. Na tutagongana tutasemana lakini turudi tukae tuelekezane tuelimishane, tujadiliane na tukubaliane twende na siasa zetu. 


 
Amani hupatikana kwa ncha ya ulimi. Na hii inaonesha umuhimu wa kukaa na kuzungumza. Tunamfano mzuri ndani ya nchi yetu. Zanzibar. Tuliamini amani inapatikana kwa ncha ya upanga, 2001 na moja tulijaribu haikuwezekana. Zanzibar mnayo iona leo amani imepatikana kwa ncha za ndimi.

Watu walikaa wakazungumza wakajadilina wakaambizana wakaelimishana. Wakasema hakuna haja tukaeni tujenge zanzibar yetu.

Nimazungumzo na sio nguvu wala ugomvi wala kutishana. Ni mazungumzo. 

Tusitazame yaliyopita tutizame tutizame mbele kwa matumaini tuweke nguvu yetu pamoja kujenga tanzania mpya yenyekusameheana kuheshimiana na kufungua kurasa mpya za kwenda na demokrasia yetu Tanzania. 


Lakini nanyi wenzangu wa vyama vya siasa muwe tayari kwenye haya kufuata sheria kujadiliana na kufikia mwafaka. Tuzike tofauti zetu za nyuma tufungue kurasa mpya za kuendesha siasa za nchi hii.

Najua kuna mengi ya kusikiliza pia, kuna madukuduku, kuna hasira malalamiko, nongwa yanayotokana na uchanga wa demokrasia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad