Mbunge wa Kuteuliwa (CCM), Humphrey Polepole amesema amepokea Mashtaka ya TCRA yanayosema kupitia Kipindi chake cha Shule ya Uongozi, amerusha Maudhui yanayopotosha Umma na yanayoweza kuchochea Watanzania kuweza kugomea Kampeni ya Kitaifa ya #COVID19
-
Akizungumza leo amesema, "Hivi mimi nimewahi kuwaambia ninyi tudhoofishe Kampeni ya Corona? Wapi niliwaambia kwa maana hiyo?"
-
Amesema kwasababu amepewa nafasi ya kujibu, atapelekea Utetezi wake aliodai unajitosheleza