Polepole Aitwa Kujieleza TCRA "Siwezi Kunyamazishwa"



MBUNGE wa kuteuliwa, Humphrey Polepole amesema ameitwa na Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kujieleza kuhusu tuhuma zinazomkabili huku akidaiwa kutoa maudhui ambayo yanaashiria uchochezi na chuki kwa Serikali kupitia mtandao wa YouTube.

Polepole amesema hayo leo Jumamosi, Desemba 11, 2021 wakati akizungumza na wanahabari katika Ukumbi wa LRHC, Kijitonyama, Dar es Salaam kufuatia maudhui ambayo amekuwa akiyatoa mitandaoni kupitia kipindi chake cha Shule ya Uongozi.

“Nimeitwa TCRA, wanasema nimetoa maudhui ya kupotosha umma yanayoweza kuchochea Watanzania kugomea na kudhoofisha kampeni ya Kitaifa kujikinga na Corona. Hivi mimi nimeshawahi kuwaambia tudhoofishe kampeni ya kujikinga na corona? hawa wanataka kunichomeka hapa.

“Sijawahi kusema kwa nini sichanji, sasa tusisukumane nikafafanua kwa nini sikutaka kuchanja. Sasa nitakwenda TCRA kupeleka utetezi wangu nikaseme ukweli maana tunatafutana kwenye korido la corona.


 
“Hii hoja ya wamachinga nasema kweli mmeonea watu, halafu mtu anasema kaa kimya, kumbe jukumu la mbunge ni nini? Sauti ya watu ni ipi? Hii kaa kimya nimehangaika nayo sana, nimefanya tu kiubishi.

“TCRA wanasema wamenipa leseni kwa ajili ya maudhui ya kipindi cha Papo kwa Hapo, wanahoji kwa nini ninafanya Shule ya Uongozi… hivi mimi nimekulipa milioni ile halafu unanipangia cha kuzungumza? naweza kuposti familia yangu au mbwa wangu, utaniuliza?

“Kuhusu corona kuna ubishi wa kidunia, kila mtu ana upande wake, na mimi niweke wazi nipo kwenye ubishi huo. Mpaka Yesu atarudi tunaendelea na ubishi,” amesema Polepole
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad