Polepole na Sakata la Kuwataja wahuni wote



Polepole ataja wahuni wote
Mbunge wa kuteuliwa na aliyekuwa katibu mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekubali kuwajibika kuhusiana na swala la wahuni serikalini akisema serikali ilikosea kuweka viongozi wanaoweza kujinasibu kuwa wao ni wahuni

Akiongea katika mahojiano maalum na Dar24 Media Polepole amesema wapo viongozi katika mitandao ya kijamii na makundi sogozi ambao wanajinasibu kuukubali uhuni.

“Hata sasa ninapokuja na huu msemo wa “Kataa wahuni” kuna viongozi wanaendelea kujinasibu kuwa wao ni wahuni ambao wamesalia kutoka awamu ya tano, uaweza ukashangaa, Mimi nakubali kuwajibika kuwa hapo tulikosea kumuweka mtu huyo katika safu ya uongozi kwa sababu haiwezekani mtu akajivuna kuwa muhuni” amesema polepole.

Alipoulizwa wahini ni kina nani haswa, Polepole amesema hawezi kuwataja kwa majina wala kuwaanisha kwa sababu vipo vyombo husika ambavyo vinatakiwa kuwafuatilia ambavyo ni Jeshi la Polisi, TAKUKURU, Taasisi ya kuzuia madawa ya kulevya, mkurugenzi wa makosa ya jinai, na mkurugenzi wa mashitaka.

“mimi niliulizwa na chombo kimoja kuhusu udhaifu wa awamu ya tano ambayo na mimi nilikuwepo na nikasema Udhaifu ni jambo gumu kulisema lakini nikikumbuka vizuri nitasema, lakini nikasema kama kuna jambo ambalo tulitamani sana liwe lakini hatukuweza kulikamilisha tukiongozwa na Rais Magufuli na mama Sami ani kuwamaliza Wahuni kwa kuwakabili na kuwachukulia hatua kali”

“Wahuni bado wapo na ni jukumu letu kuwadhibiti kuwakabili na kuwachukulia hatua kali, na wote watachukuliwa hatua na vyombo nilivyotaja hapo juu, ila niliwataja kuwa wahuni ni watu wenye tabia na mienendo yao inakwenda kinyume na Tunu zetu za taifa” alisema Polepole

Ameongeza kuwa wahuni ni wabadhilifu wa mali za umma, wala rushwa, watoa rushwa, watumiaji wa mali za serikali na chama cha mapinduzi na wahuni hawa wapo ndani ya serikali, chama cha mapinduzi na nje ya chama, hawasikilizi wananchi wao akifafanua kuwa mtu anapopewa kazi ya uongozi na asiskilize shida zao ni muhuni tu

“Mimi kama mtanzania raia makini na ninaeipenda nchi yangu naendelea kusema kwangu mimi watu kama hawa hawakubaliki na hawana nafasi katika Maisha ya watanzania na ni vikwazo na wanachelewesha neema, haki na maslahi mapana ya kimaendeleo kwa watanzania, hao ni vikwazo” amesema Polepole

Humphrey Polepole hivi karibuni amekua na msemo wa “kataa wahuni” na ameuendeleza katika mitandao yake ya kijamii

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad