Polisi afika kazini akiwa mlevi, kumuua bosi wake na kutoroka



Afisa mmoja wa polisi Naivasha amuua kwa kumpiga risasi bosi wake aliyemuuliza mbona alifika kazini kwa kuchelewa tena akiwa mlevi
Joseph Muthunga alimmiminia risasi Ayub Polo kabla ya kukimbilia mafichoni huku makachero wakianza msako dhidi yake
Mabaki matano ya risasi yalipatikana eneo la tukio hilo lilitokea katika kambi ya AAPS eneo la Kedong, Naivasha
Makachero mjini Naivasha wameanzisha msako mkali wakilenga kumnasa afisa mmoja wa polisi aliyemuua mwenzake kwa kumpiga risasi katika kambi ya AAPS kule Kedongo usiku wa Jumamosi kabla ya kutoroka.a

Naivasha: Polisi Mlevi Amuua Bosi Wake kwa Kumpiga Risasi na Kutoroka
Joseh Muthunga alimmiminia risasi Ayub Polo kutumia bunduki ya G3 (pichani) kabla ya kutoroka. Picha: Nairobi News
Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, afisa huyo kwa jina Joseph Muthunga alifika kambini akiwa mlevi na kuzua ugomvi na afisa mwenzake Sajenti Ayub Polo baada ya kuulizwa mbona alirejea kambini kwa kuchelewa ilhali alistahili kuwa kazini usiku huo.

Ugomvi huo ulitokea kuwa mkali sana ndipo Muthunga alipochukua bunduki aina ya G3 na kummiminia risasi Sajenti Polo kabla ya kukimbilia mafichoni.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, mwili wa marehemu ulikuwa na majeraha ya risasi kwa sikio, bega na goti.


 
Mabaki ya risasi tano yalipatikana katika eneo la tukio.

Mwili wa mwendazake umepelekwa katitika hifadhu ya maiti ya Umme mjini Mai Mahiu unakosubiri kufanyiwa upasuaji.

Katika taarifa inayofungamana na hii, TUKO.co.ke iliripoti mnamo Disemba 7, 2021 kuwa afisa mmoja wa polisi aliyekuwa akihudumu katika kituo cha polisi cha Kabete kaunti ya Kiambu aliwaua watu sita kabla ya kujiua mwenyewe.


Polisi huyo kwa jina Benson Imbatu anasemekana kuhusika katika vita na mkewe kwa jina Carol kabla ya kumuua kwa kumpiga risasi.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, jirani ya wawili hao alisikia mlio mkubwa wa kitu kikigongwa kisha mlio wa risasi, hali liyomfanya kukimbia katika kituo cha polisi cha Kabete kupiga ripoti.

Maafisa wa polisi walifululiza hadi eneo la tukio ndipo ikajulikana kuwa afisa huyo alikuwa amemuua mkewe kwa kumpiga risasi shingoni.

Akiwa amejihami kwa bunduki aina ya AK47, Imbatu alianza kumimina risasi kiholela, akiwaua watu wengine watano wakiwemo wahudumu wawili wa bodaboda.


 
Mmoja wa wahudumu wa bodaboda akifariki akipokea matibabu katika Hospitali Kuu ya Kenyatta.

Watu wengine wawili walipata majeraha na kukimbizwa katika Hospitali Kuu ya Kenyatta ambako wanaendelea kupata nafuu.

Baadaye afisa huyo alijiuua kwa kujipiga risasi shingoni vilevile.

Maafisa wa polisi walichukua bunduki iliyotumiwa kutekeleza unyama huo ambao ulithibitishwa na kamanda wa Polisi Francis Wahome.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad