Maelezo ya picha, Sheikh Mohammed Bin Rashid Al-Maktoum na mtalaka wake, Binti Mfalme Haya Bint Al-Hussain
Inaelezwa kuwa ndio kesi kubwa zaidi ya talaka katika historia ya sheria nchini Uingereza makubaliano ya kiasi cha zaidi ya pauni milioni 500 inayomhusisha bilionea na mtawala wa Dubai na mkewe waliyeachana naye.
Mahakama Kuu ya Uingereza siku ya Jumanne imeamuru jumla ya malipo ya mkupuo wa paundi milioni 251.5 yatolewe kwa binti wa mfalme zamani wa Jordan Hussein, Haya Bint Al-Hussain mwenye umri wa miaka 47.
Haya Bint Al-Hussain ndiye mke mdogo kati ya wake sita wa Sheikh Mohammed Bin Rashid Al-Maktoum, Bilionea na mtawala wa Dubai, Waziri mkuu wa UAE na mmiliki wa shindano la mbio za farasi
Hukumu hiyo inampa Binti mfalme Haya pesa kwa ajili ya kufidia gharama ya kuendesha nyumba mbili za kifahari, moja ipo karibu na makazi ya kifalme katika Kasri ya Kensington mjini London na nyingine ni makazi yake yaliyopo Egham, Surrey.
Malipo hayo pia yamejumuisha bajeti kwa ajili ya usalama, likizo, mishahara na malazi kwa waaguzi na yaya, magari ya kivita ya familia na gharama za kutunza farasi na wanyama wa nyumbani
Pia imeruhusu malipo ya pauni milioni 5.6 kwa mwaka kwa kila mmoja wa watoto wake wawili, binti wa miaka 14 na mtoto wa kiume wa miaka tisa. Hizi zitalindwa na dhamana ya pauni millioni 290.
'Hofu ya maisha yake'
Kesi hii ya iliyoendeshwa kwa muda mrefu imetoa mwangaza katika ulimwengu wa familia za kifalme ambazo kawaida hufungwa
Binti mfalme Haya alikimbia kutoka Dubai kwenda Uingereza na watoto wake mwaka 2019, akisema alikuwa na hofu ya maisha yake, baada ya kugundua Sheikh Mohammed alikuwa amewateka nyara mabinti zake wengine wawili ambao ni Sheikha Latifa na Sheikha Shamsa - na kuwarudisha Dubai kinyume na matakwa yao.
Sheikh Mohammed, 72, ambaye pia ni mtu mkubwa katika ulimwengu wa mbio za farasi, alikanusha utekaji nyara huo licha ya hukumu ya Mahakama Kuu ya 2020 kusema kuwa, kuna uwezekano na ukweli.
Alichapisha shairi lililoitwa "Umeishi, Umefariki", ambalo lilidhaniwa ni kumtishia binti mfalme baada ya kugundua kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mlinzi wake wa zamani.
Binti mfalme Haya aliendelea kupokea vitisho baada ya kuhamia Uingereza huku baadhi ya jumbe zikisema "tunaweza kukufikia popote" na tangu wakati huo ametumia pesa nyingi kulinda usalama kwa kuhofia watoto wake kutekwa na kurudishwa Dubai.
Mfalme wa Dubai na mkewe aliyetoroka mahakamani
UAE yaunda wizara mpya ya 'furaha'
Haya fled alitoroka Dubai na kwenda Uingereza na watoto wake mwak 2019, akisema nahofia maisha yake
Mahakama Kuu imetoa maamuzi mwaka huu kwamba Sheikh Mohammed alidukua kinyume cha sheria simu za Binti mfalme Haya, walinzi wake na timu yake ya wanasheria, ambayo ni pamoja na Tory peer Baroness Shackleton.
Udukuzi huo ulifanywa kwa kutumia programu ya kudukua iitwayo Pegasus, ambayo huingia katika simu zinazolengwa, program hiyo ilitengenezwa na kampuni ya Israel ya NSO Group.
Kuhusu binti mfalme Haya, aliongeza kuwa "ataendelea kuwa katika hatari kwa muda uliobaki wa maisha yake, iwe kutoka kwa Sheikh Mohammed au kutoka kwa gaidi wa kawaida na vitisho vingine."
Binti wa mtawala wa Dubai aliyetoweka
Jinsi Dubai ilivyokuwa jiji linalong’aa lenye maghorofa marefu katika miaka michache
Mahakama iliambiwa juu ya tathmini ya usalama ambayo inawaweka katika hatari binti mfalme Haya na watoto wake kuwa ni kali mno. Baadaye hakimu akatoa jumla ya kiasi cha fedha za kulipia gharama za uendeshaji wa magari ya kivita kwa ajili ya kusafirisha familia.
Jaji wa Mahakama Kuu anasema amejitahidi kadiri awezavyo kufikia uamuzi unaofaa, kutokana na mali na kiwango cha maisha ambacho watoto walikuwa wakiishi wakati wa ndoa.
Mawakili wa binti mfalme Haya walisisitiza kuwa hakutoa madai yoyote kwa mahitaji yake ya baadaye lakini alikosolewa wakati wa vikao vya mahakama kwa matumizi yake ya kifahari, kwa mfano, Mwanae mwenye umri wa miaka tisa pekee, amepewa magari matatu ya bei ghali kwa vile alikuwa amezoea kupewa magari kama zawadi.
Maelezo ya picha, Sheikh Mohammed, 72, ni waziri mkuu na mtu mkubwa katika ulimwengu wa mbio za farasi
Hukumu hiyo ni imejumuisha ushahidi uliotolewa na binti mfalme Haya kuwa alitishwa na wafanyakazi wake wa usalama kutokana na uhusiano wa kimapenzi aliokuwa nao na mmoja wao.
Alifanya malipo kadhaa kwa wafanyikazi wanne, baadhi ya malipo yalitoka kwenye akaunti za benki za watoto wake Ili kurekebisha hili. Anasema aliuza vito vya thamani ya zaidi ya Pauni milioni 1 na tangu wakati huo alilazimika kuuza vito zaidi.
Sheikh Mohammed wa Dubai amesema vitu vya urithi alivyopewa mke wake huyo wa zamani vitatumwa kwake, ikiwa ni pamoja na viatu vya ballet aliyopewa na wachezaji maarufu duniani Dame Margot Fonteyn na Rudolf Nureyev. Pia alisema ameondoa shairi la mtandaoni alilohusishwa ambalo binti mfalme aliliona kuwa tishio kwa maisha yake