Na @johnharamba
Unapotaja majina ya wasanii ambao unaamini ni wakali katika muziki wa Hip Hop na Bongo Fleva kwa miaka 15 iliyopita, amini kuwa katika orodha hiyo utakayotaja huwezi kuacha kulitaja jina la Profesa Jay.
Lakini cha kufurahisha zaidi ni kuwa hata hao wote utakaowataja katika orodha hiyo nina uhakika asilimia 95 au 100, wote watakuwa pia walikuwa inspired na Profesa Jay.
Kumbuka nyuma ya miaka hiyo 15 wapo waliokuwa sahani moja na Jay wakati akiwa kwenye ubora wa juu, huko nako kuna wasanii wengi waliingia kwenye fani ya muziki kwa sababu ya kile kilichokuwa kikifanywa na Profesa Jay.
Yaani kwa ufupi @professorjaytz ni role model wa role models wa wasanii kibao.
Jay ni mwanasiasa lakini binafsi naamini huyu mwamba alizaliwa kwa ajili ya muziki. Sijawahi kuwa shabiki wake katika masuala ya siasa, lakini katika muziki ni mfalme wa wafalme.
Sasa pamoja na kuwa kwa zaidi ya miaka 20 amefanya muziki, uliompa umaarufu na mambo mengine kibao, ajabu ni kuwa ameendelea kubadilika kulingana na muda, utamu wake hata kama umepungua lakini siyo katika kiwango cha kumuona kama wale wazee ving’ang’anizi wa game huku wakiwa hawana uwezo.
Ndiyo wapo wasanii wengi tu ambao uwezo wao unaona kabisa umefika mwisho, lakini kwa kuwa hawakujipanga kimaisha, wanalazimisha kutaka jamii iwaone wao bado ni wasanii wakali, wanachokifanya hakiendani na kizazi cha sasa, mwisho wanaishia kulaumu watu tu kila siku.
Jay wa sasa anapiga kolabo na wajukuu zake kwenye game kina Young Lunya.
Tazama nguo anazovaa, prodyuza anaofanya nao kazi, michano yake anai upgrade kila kukicha, flow zake zinaenda na kizazi cha sasa, make up wakati wa kushoot ni ya kisasa, quality ya video ni bomba n.k.
Kwa ufupi Jay ni definition of Bongo Fleva, yaani ni tafsiri halisi ya muziki huo, anachokifanya Joseph Haule ni kama kinachofanywa kule Bollywood (India) na @amitabhbachchan, jamaa kama kinyonga kila kizazi yupo.
Asante Jay huu ni muda wa kuiinjoy goma la HANDS UP' Ft @gnakowarawara .