Rais Ramaphosa akabidhi majukumu yake




Rais wa Arika Kusini Cyril Ramaphosa amekabidhi majukumu yake yote kwa Naibu Rais David Mabuza, baada ya kupimwa na kukutwa na Covid-19 na anatibiwa kwa dalili zisizo kali.

Taarifa kutoka Ofisi ya Rais imesema kuwa Rais Ramaphosa ameanza kujisikia vibaya siku ya Jumapili baada ya kuondoka katika ibada ya kumbukumbu ya Rais wa mwisho wa enzi za ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini FW De Klerk mjini Cape Town.

Watu ambao walikuwa karibu na Rais siku hiyo wameshauriwa kutazama dalili lakini pia kupimwa.

Aidha Rais Ramaphosa amepewa chanjo kamili.


 
Rais Ramaphosa amerejea Jumatano iliyopita kutoka katika ziara ya nchi za Afrika Magharibi za Nigeria, Ivory Coast, Ghana na Senegal.

Rais amesema yeye na wajumbe wake walipimwa Covid katika nchi zote walizotembelea, ambapo taarifa hizo zinasema Rais amepatikana bila virusi hivyo aliporejea.

Kirusi cha Omicron kinachoambukiza sana, ambacho kimezua wasiwasi wa kimataifa, kilitambuliwa kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini mwezi uliopita.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad