Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameyaonya makundi yanayochafua Serikali yake ya awamu ya sita kwa kusema kuwa ufisadi umerudi na mambo yako hovyo.
Akizungumza leo Jumamosi Desemba 4, 2021 wakati akizindua gati katika Bandari ya Dar es Salaam, amesema kuna makundi ndani ya Serikali wanajua wanayoyafanya ingawa yanageuka na kusema Serikali hii ya awamu ya sita ufisadi umerudi.